MASOMO YA LEO JUMAMOSI JUMA LA 22 LA MWAKA 9 SEPTEMBA 2017
SOMO1:Kol.1:21-23
Ninyi mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa,tena adui katika nia zenu,kwa matendo yenu mabaya,amewapatanisha sasa;katika mwili wa nyama yake kwa kufa kwake,ili awalete ninyi mbele zake,watakatifu wasio na mawaa wala lawama;mkidumu tu katika ile imani,hali mmewekwa juu ya msingi,mkawa imara, msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake,iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu;ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake.
K:Mungu ndiye anayenisaidia.-Zab.54:1-2,4,6
INJILI:Lk.6:1-5
Ilikuwa siku ya sabato moja Yesu alikuwa akipita katika mashamba,wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke ya kuyala,wakiyapukusa-pukusa mikononi mwao.Basi baadhi ya Mafarisayo wakawaambia,Mbona mnafanya lisilo halali siku ya sabato?Yesu akawajibu akawaambia,Hamkulisoma hata hilo alilolifanya Daudi,alipokuwa na njaa,yeye na wale waliokuwa nao?Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu,akaitwaa mikate ile ya Wonyesho,akaila akawapa na hao wenziwe,ambayo si halali kuila ila kwa makuhani peke yao.Akawaambia,Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.

No comments: