Wednesday, April 2 2025

SALA YA JIONI NA SALA KWA AJILI YA SHIDA KUBWA.

Sala ya jioni.
Tunakushuru,ee Mungu,kwa mapaji yote uliyotujalia leo.Amina.

Baba yetu.
Baba yetu uliye mbinguni,jina lako litukuzwe.Ufalme wako ufike.Utakalo lifanyike,duniani kama mwbinguni.Utupe leo mkate wetu wa kila siku.Utusamehe makosa yetu,kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.Usitutie katika vishawishi ,lakini ukuopoe maovuni.Amina.

Salamu Maria
Salamu,Maria,umejaa neema Bwana yu nawe,umebarikiwa kuliko wanawake wote,na yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria mtakatifu mama wa Mungu,utuombee sisi wakosefu,sasa na saa ya kufa kwetu.Amina.

Sala ya mapendo.
Mungu wangu,
nakupenda kwa moyo wangu wote,kwani wewe unayo mema yote.Nampenda na binadamu mwenzangu kama nafsi yangu,kwa kuwa wewe ni baba wa watu wote.Amina.

Sala kwa ajili ya shida kubwa
Sala hii yaweza kutumika pia kama novena ya siku 9 kwaajili ya shida kubwa.

EeMtakatifu Rita wa mambo yaliyoshindikana na mwombezi wa waliokata tamaa,nakuja kwako kuimba unisikilize na kunisaidia katika shida yangu hii kubwa.Najua kuwa wewe ni mwombezi wa shida kubwa na msaada wa waliokata tamaa,basi nakuomba dhihirisha uwezo na nguvu yako kwa kunijalia kwa mungu hitaji langu(hapa omba hitaji unalotaka Mungu akujalie kupitia maombezi ta Mt.Rita wa kashia).
Wewe unajua mahangaiko na maumivu yangu,njoo hima,Ee Rita unisaidie.Ninaamini kuwa ombi langu litapata suluhisho na shida yangu itakwisha kabisa kupitia maombezi yako yenye nguvu.Ee Mtakatifu Rita wa kashia mwombezi wa shida kubwa,uniombee.Amina.
Baba yetu×3
Salamu Maria×3 na 
Atukuzwe Baba×3.

32 comments:

  1. Mungu ni mwema.... Azidi kutupigania dhudi ya adui mwovu shetani...Amen

    ReplyDelete
  2. Mungu ni mwema.... Azidi kutupigania dhudi ya adui mwovu shetani...Amen

    ReplyDelete
  3. Mwenyezi Mungu baba asante kwa mavuno uliyonijalia mwaka huu 2018.Naja kwako baba kwa baraka zako unijalie soko la mashudu mahindi na mafuta ya alizeti lenye bei nzuri itakayorudisha Ghar ama zauzalishaji na kupata faida nitakayo wekeza katika msimu wa kilimo mwaka 2019 Amina

    ReplyDelete
  4. thanks so much ma God bleessing you becz we are knowing things through this wwkpedia

    ReplyDelete
  5. Amina ,Ewe mtakatifu Wa kashia utuombee

    ReplyDelete
  6. Mtakatifu Rita wa Kashia hujawahi kuniacha hujawahi aacha kuniombea fadhila kwa Yesu mchumba wako wa kimbingu...Nashukuru kwa neema hio Amina

    ReplyDelete
  7. Mtakatifu Ritha hajawahi kuniacha Nina shuhuda nyingi sana katika maisha yangu hakuna niombalo lisiwe asante Mungu

    ReplyDelete
  8. Eee mtakatifu Rita wa Akashia naomba unijalie hitaji la moyo wangu,Amina

    ReplyDelete
  9. Ee mtakatifu Rita wa kashia naomba unijalie amani ya moyo kwa kunijibu hitaji la moyo wangu.

    ReplyDelete
  10. Ee Rita mtakatifu wa mambo yalioshindika naomba unijalie niweze kushida majaribu yanayonikabili katika maisha yangu ya kila siku na katika ndoa yangu.

    ReplyDelete
  11. Nina Imani kubwa na Mungu, ee mtakatifu Rita niombee.... nipate kibali.

    ReplyDelete
  12. Ee mtakatifu Rita wa Kashia nijalie niweze kuyashinda haya majaribu yanayonikumba. Amina

    ReplyDelete
  13. Eeeh Mtakatifu Ritha, naomba unisaidie niwez kupata ela yangu ya kodi, kapla tarehe 15(mwezi huu wa pili) na Pia unisaidie katik masom yang niwez kufaulu vizuri, nisipate supp, na pia nisaidie kupata sehem nzuri ya field, na pia usiache barak nyingi za kupata ela na connection.

    ReplyDelete
  14. Asante Mungu, Asante Yesu, asante mt. Rita wa Kashia kwa muujiza uliotenda kwangu, lililoshindikana kwa miaka sita, ukalijibu ndani ya mwezi mmoja. Huu muujiza utanikumbusha maombezi yako daima. hakika ni mama muombezi wa shida kubwa maishani

    ReplyDelete
  15. Nina Imani na matumaini kwako Mt Ritha wa kashia Mara zote hukuniacha naomba pia msaada wako kwa hili nikuambalo Ili niendelee kutoa ushuhuda wako kwa wasiokujua bado

    ReplyDelete
  16. Eee mt. Ritha naja mbele zako kuomba suluhisho juu ya masomo yangu najua kwako hakuna kisicho shindikana amina .

    ReplyDelete
  17. Eee Mt Rita wa mambo yaliyoshindikana, kwa unyenyekevu mkubwa nasubiri majibu ya maombezi yako kwa Mungu kwa maombia ya shida nilizokuomba. Nina imani unazidi kuniombea kwa Baba ili ndani ya muda mfupi niweze kupewa majibu ya shida zangu nilizozipitishia kwako kwenda kwa Mungu. Ninayo imani nitajibiwa.

    ReplyDelete
  18. Siku ya Saba Mtakatifu Ritha muombezi wetu kwa yale yaliyoshindikana uniombee kwa Yesu niweze kupata kazi nzuri.Amina

    ReplyDelete
  19. Ee mtakatifu rita wa kashia naomba unijalie amani ya moyo na uniombee kwa Mungu anisamehe makosa yangu na anisaidie katika shida yangu hii kubwa

    ReplyDelete
  20. Ee Mtakatifu rita wa kashia naomba unijalie Mchumba Mwema wa maisha yangu ,niombee kwa Mungu wetu nisamehe Dhambi zangu anipe Amani na nguvu ya kulitangaza jina lake popote Duniani Amina.

    ReplyDelete
  21. Ee Mt Rita nanyenyekea mbele zako unisaidie shida zangu unifungulie njia zenye baraka maishani mwangu nakuomba unisikilize

    ReplyDelete
  22. Mt Ritha nakuja mbele zako nakuletea shida zangu zinazovunja moyo wangu uniombee ili niweze kuzitatua kwa muda mfupi amen

    ReplyDelete
  23. Mt.Rita wa Kashia muombezi wa mambo yalioshindikana nakuomba kwa unyenyekevu mkubwa sana Napitia changamoto kubwa na nzito sana JUU YA MASOMO YANGU Hapa UDOM ,naomba weka mkono wako nivuke salama nimengi ya kukatisha Tamaa na mengi yamesemwa juu yangu naomba nipate suluhisho la masomo yangu ya UDAKTARI

    ReplyDelete

Powered by Blogger.