MASOMO YA LEO ALHAMISI JUMA LA 19 LA MWAKA 17 AGOSTI 2017

SOMO1:Yos.3:7-11,13-18


Bwana alimwambia Yoshua,Hivi leo nitaanza kukutukuza mbele ya Israeli wote,wapate kujua ya kuwa mimi nitakuwa pamoja na wewe,kama nilivyokuwa pamoja na Musa.Nawe uwaamuru hao makuhani walichukuao sanduku la agano,ukawambie,mtakapofika ukingo ya maji ya Yordani,simameni katika Yordani.Basi Yoshua akawambia wana wa Israeli,njoni huku,mkayasikie maneno ya Bwana Mungu wenu,Yoshua akasema,kwa jambo hili mtajua ya kuwa Mungu aliye hai yu kati yenu,na ya kwa kuwa hata kosa kuwatoa mbele mbele yenu Mkaanani,na Mhiti,na Mhivi,na Mperizi na Mgirgashi,na Mwamori,na Myebusi. Tazama sanduku la agano la Bwana wa dunia yote linavuka mbele yenu na na kuingia Yordani. Itakuwa wakati nyayo za makuhani walichukuao sanduku la Bwana,Bwana wa dunia yote zitakaposimama katika maji ya Yordani,hayo maji ya Yordani yatatindika,maji yale yashukayo kutoka juu;nayo yatasimama kama chuguu.Hata ikiwa hao watu walipotoka katika hema zao,ili kuvuka Yordani,makuhani walichukua sanduku la agano wakatangulia mbele ya watu,basi hao walipochukua hilo sanduku walipofika Yordani,na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni,(maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno) ndipo hayo maji yalishuka kutoka juu yakasimama,yakainuka,yakawa chuguu,mbali sana,huko Adamu,mji ule ulio karibu na sarethani,na maji yale yaliyoteremkia bahari ya Araba,yaani bahari ya chumvi,yakatindika kabisa;watu wakavuka kukabili Yeriko.Na hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la Bwana wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Yordani;Israeli wote wakavuka katika nchi kavu,hata taifa lile lote likaisha kuvuka Yordani.

K:Aleluya. -Zab.114:1-6

INJILI:Mt.18:21-19:1

Petro alimwendea Yesu akamwambia,Bwana,ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe?Hata mara saba?Yesu akamwambia,Sikambii hata mara saba,bali hata saba mara sabini.Kwasababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.Alipoanza kuifanya,aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi.Naye alipokosa cha kulipa,bwana wake akaamuru auzwe,yeye na mke na watoto wake,na vitu vyote alivyo navyo ili akalipe deni.Basi yule mtumwa akaanguka,akamsujudia akisema,Bwana,nivumilie,nami nitakulipa yote pia.Bwana wa mtumwa akamhurumia,akamfungua,akamsamehe ile deni.Mtumwa yule akatoka akamwona mmoja wa wajoli wake,aliyemwia dinari mia;akamkamata,akamshika koo,akisema,Nilipe uwiwacho.Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake,akamsihi akasema,Nivumilie nami nitakulipa yote pia.Lakini hakutaka,akaenda,akamtupa kifungoni,hata atakapoilipa ile deni.Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka,walisikitika sana,wakaenda wakamweleza Bwana wao yote yaliyotendeka.Ndipo bwana wake akamwita akamwambia,Ewe mtumwa mwovu,nalikusamehe wewe deni yote,uliponisihi;nawe,je!Haikupasa kumrehemu mjoli wako,kama mimi nilivyokurehemu wewe?Bwana wake akaghadhabika,akampeleka kwa watesaji,hata atakapolipa deni ile yote.Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi,msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo,akatoka Galilaya akafika mipaka ya Uyahudi,ng'ambo ya Yordani. 

No comments:

Powered by Blogger.