MASOMO JUMA LA 19 LA MWAKA 18 AGOSTI 2017

SOMO1:Yos.24:1-13

Yoshua aliwakusanya kabila zote za Israeli huko Shekemu,akawaita wazee wa Israeli,na wakuu wao,na waamuzi wao,na maakida wao;nao wakahudhuria mbele za Mungu. Yoshua akawambia watu wote:Bwana,Mungu wa Israeli,asema hivi Baba zenu hapo zamani walikaa ng'ambo ya Mto,maana Tera,baba yake Ibrahimu,naye ni baba yake Nahori,wakaitumikia miungu mingine.Nami nikamtwaa Ibrahimu baba yenu toka ng'ambo ya Mto,nikamwongoza katika nchi yote ya kaanani;nikaongeza uzao wake,nikampa Isaka. Kisha nikampanhuyo Isaka Yakobo na Esau;nami nikampa Esau mlima Seiri aumiliki;Yakobo na watoto wake wakashka Misri. Kisha nikawatuma Musa na Haruni,nikaipiga nchi Misri,kwa hayo yote niliyatenda kati yake;hatimaye nikawatoa ninyi.Nikawatoa baba zenu watoke Misri,nanyi mkaifikilia habari;Wamisri,wakawafuata baba zenu kwa magari na wapanda farasi mpaka bahari ya shamu.Nao walipomlilia bwana akaweka giza kati ya ninyi na wa Misri,akaileta bahari juu yao,akawafunikiza;nayo macho yenu yalipoona mambo niliyoyatenda huko Misri.;kisha mkakaa jangwani siku nyingi.Kisha nikawaleta na kuwaingiza katika nchi ya Waamori,waliokaa ng'ambo ya pili ya Yordani;nao wakapigana nanyi;nikawayia mikononi mwenu, mkaimiliki nchi yao;nami nikawaangamiza mbele yenu.Ndipo Balaki,mwana wa sipori,Mfalme wa Moabu,akainuka,akapigana na Israeli;tena akatuma watu akamwita Balaamu,mwana wa Beori,aje awalaani;lakini sikukubali kumsikiliza Balaamu,kwahiyo akafuliza kuwabariki ninyi;nikawatoa katika mkono wake.Nanyi mliuvuka Yordani,mkafika Yeriko;nao watu wa Yeriko wakapigana nanyi,Mwamori,na Mperizi,na Mkaanani na Mhiti,na Mgirgashi,na Mhivi,na Myebusi;nami nikawatia mikononi mwenu.Nikatuma mavu mbele yenu,waliowafukuza mbele yenu hao wafalme wawili wa Waamori,si kwa upanga wako,wala upinde iwako.Nami nimewapa ninyi nchi msiyoitendea kazi,na miji msiyoijenga,nanyi mmekaa humo;mnakula matunda ya mashamba ya mizabibu na miziituni msiyoipanda.

K:Maana fadhili zake niza milele.-Zab.136:1-4,16-18,21-22

INJILI:Mt.19:3-12

Mafarisayo walimwendea Yesu wakamjaribu,wakamwambia,Je! Ni halali mtu kumwacha mke kwa kila sababu?Akajibu,akawaambia,Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo aliwaumba mtu mume na mtu mke,akasema,kwa sababu hiyo,mtu atamwacha babaye na mamaye,ataambatana na mkewe;na hao wawili watakuwa mwili mmoja?Hata wamekuwa si wawili tena,bali ni mwili mmoja.Basi aliowaunganisha Mungu,mwanadamu asiwatenganishe.Wakamwambia jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka,na kumwacha?Akawaambia,Musa,kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu,aliwaparuhusa ya kuwaacha wake zenu,lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.Nami nawaambia ninyi,kila mtu atakayemwacha mkewe,isipokuwa kwa sababu ya uasherati,akaoa mwingine,azini;naye amwoaye yule aliyeachwa azini.Wanafunzi wake wakamwambia,Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo,haifai kuoa.Lakini yeye akawaambia,Si wote wawezao kulipokea neno hili,ila wale waliojaliwa.Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao;tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi;tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni.Awezaye kulipokea neno hili na alipokee.

No comments:

Powered by Blogger.