TUANZE SIKU NA BWANA KWA KUTAFAKARI PAMOJA MASOMO YA 7/7/2017.

Sala ya Asubuhi.
Kwa jina la Baba na la Mwana,na la Roho Mtakatifu.Amina.

Ee Baba yetu mungu mkuu,
Umemilinda usiku huu,
Nakushukuru kwa moyo,
Ee Baba Mwana na Roho,
Nilinde tena siku hii,
Niache dhambi nikutii,
Naomba sana,Baba we,
Baraka yako nolipokee,
Bikira safi ,Ee maria,
Nisipotee nisimamie,
Mlinzi mkuu Malaika we,
Kwa Mungu wetu niombee,
Nitake nitende mema tu,
Na mwisho nije kwako juu.Amina.

SOMO 1:Mwa.23:1-4,19;24:1-8,62-67.
Umri wake Sara ulikua miaka mia na ishirini na saba,ndio umri wake Sara.Sara akafa katika kiriatharba,ndio hebroni,katika nchi ya kaanani Ibrahimu akaja kumlilia Sara na kumwombolezea.Akaondoka Ibrahimu kutoka mbele ya maiti wake,akasema na bana Hethi,akinena,Mimi ni mgeni,ninatembea kwenu,nipeni mahali pakuzika kwenu,pawa pangu,nimzike maiti wangu atoke mbele yangu.Basi baada ya hayo Ibrahimu akamzika na Sara mkewe katika pango la shamba la Makpela kuelekea Mamre,ndiyo Hebroni,katika nchi ya kaanani.Ibrahimu alikua mzee mwenye miaka mingi sana,na Bwana alikua amembariki Ibrahimu katika vitu vyote.Ibrahimu akamwambia mtumishi wake,mzee wa nyumba yake,aliyetawala vitu vyake vyote,tafadhali utii mkono wako chini ya paja langu,nami nitakuapisha kwa Bwana,Mungu wa mbingu,na Mungu wa nchi,kwamba hutamtwalia mwanangu mke katika binti za Wakaanani ambao nakaa kati yao;bali enenda hata nchi yangu,na kwa jamaa zangu,ukamtwalie mwanangu Isaka mke.Yule mtumishi akamwambia,Labda mwanamke hatakubali kufuatana nami mpaka nchi hii,je!Nimrudishe mwanao mpaka nchi ulipotoka?Ibrahimu akamwambia, ujihadhari,usimrudishe mwanangu huko.Bwana Mungu wa mbinguni,alinitoa katika nyumba ya babaangu na kusema nami katika nchi niliyozaliwa,aliniapia akisema,Nitawapa uzao wako nchi hii;yeye atampeleka malaika wake mbele yako,nawe utamtwalia mwanangu mke tokea huko;na yule mwanamke asipokubali kufuatana nawe,basi,utamfunguliwa kiapo changu hiki;lakini usimrudishe mwanangu.Basi Isaka alikua amekuja kwa njia ya Bar-lahai-roi,maana alikaa katika nchi ya kusini.Isaka akatoka ili kutafakari kondeni wakati wakati wa jioni;akainua macho yake,akaona,kuna ngamia wanakuja.Rebeka akainua macho,naye alipomwona Isska,alishuka juu ya ngamia.Akamwambia mtumishi ni nani mtu huyu ajaye kondeni kutulaki?Mtumishi akasema,Huyu ndiye bwana wangu.Basi akatwaa shela yake akajifunika.Yule mtumishi akamwambia Isaka mambo yote aliyotenda.Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake,Sara,akamtwaa Rebeka,akawa mkewe;kampenda Isaka akafarijika kwa ajili kufa kwa mama yake.

K:Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema.-Zab.106:1-5

INJILI:Mt.9:9-13.
Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani,aitwaye Mathayo,akamwambia,Nifuate.Akaondoka akamfuata.Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula,tazama,watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake.Mafarisayo walipoona,waliwaambia wanafunzi wake,Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?Naye aliposikia,aliwaambia,wenye afya hawahitaji taabibu,bali walio hawawezi.Lakini nendeni,mkajifunze maana yake maneno haya,Nataka rehema,wala si sadaka;kwa maana sikuja kuwaita wenye haki,bali wenye dhambi.

2 comments:

Powered by Blogger.