TUTAFAKARI PAMOJA MASOMO YA TAREHE 6/7/2017 ALHAMISI JUMA LA 13 LA MWAKA.

SOMO1:Mwa.22:1-19
Mungu alimjaribu
Ibrahimu,akamwambia,Ee Ibrahimu naye akasema,Mimi hapa.Akasema,umchukue mwanao,mwana wako wa pekee,umpendaye,Isaka,ukaende zako mpaka nchi ya Moria,ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmoja wapo nitakaokuambia.Ibrahimu akaondoka alfajiri,akatandika punda wake,akachukua vijana wawili pamoja naye,na Isaka mwanawe,akachanja kuni kwaajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa,akaondoka,akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.Siku ya tatu Ibrahimu akainua macho yake,akapaona mahali pakali mbali.Ibrahimu akawaambia vijana wake,kaeni ninyi hapa pamoja na punda,na mimi na kijana tunakwenda kule,tukaabudu na kuwarudia tena.Basi Ibrahimu akazitwaa kuni za hiyo sadaka,akamtwika Isaka mwanawe;akatwaa moto na kisu mkononi mwake,wakaenda wote wawili pamoja.Isaka akasema na Ibrahimu baba yake,akinena,Babaangu!Naye akasema,Mimi hapa mwanangu.Ibrahimu akasema,Tazama!Moto upo,na kuni zipo,lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa hiyo sadaka ya kuteketezwa?Ibrahimu akasema mungu,Mungu atajipatia mwana kondoo kwa hiyo sadaka,mwanangu.Basi wakaendelea wote wawili pamoja.Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu,Ibrahimu akajenga madhabahu huko ,akaziweka tayari kuni,kisha akamfunga isaka mwanae,akamweka juu ya madhabahu,juu ya zile kuni.Ibrahimu akaonyesha mkono wake, akitwaa kisu ili amchinje mwanawe.Ndipo malaika wa bwana akamwita kutoka mbinguni,akasema,Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema,Mimi hapa.Akasema usimnyooshee kijana mkono wako,wala usimtendee neno;kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu,iwapo hukunizuilia mwanao,mwanao wa pekee.Ibrahimu akainua macho yake,akaangalia,na tazama,kondoo mume yuko nyuma yake,amenaswa pembe zake katika kichaka.Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo,akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.Ibrahimu akaita mahali hapo Yehova-yire,kama watu wasemavyo hata leo,katika mlima wa Bwana itapatikana.Malaika wa Bwana,kwa kuwa umetenda neno,wala wala hukunizuilia mwanao,mwanao wa pekee,katika kubariki nitakubariki,na katika kuzidisha nitaudisha uzao wako kama nyota za mbinguni,na kama mchanga ulioko pwani;na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;na katika uzao wako mataifa yote ya duniani watajibarikia;kwa sababu umetii sauti yangu.Basi Ibrahimu akawarudia vijana wake,wakaondoka,wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba.Ibrahimu akakaa huko Beer-sheba.

K:Nitaenenda mbele za Bwana katika nchi za walio hai.-Zab.116:1-6,8-9.

INJILI:Mt.9:1-8
 Yesu alopanda chomboni,akavuka,akafika mjini kwao.Na tazama,wakamletea mtu mwenye kuooza,amelala kitandani;naye Yesu,alipoiona imani yao,alimwambia yule mwenye kupooza,Jipe moyo mkuu,mwanangu;umesamehewa dhambi zako.Na tazama,baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao,Huyu anakufuru.Naye yesu hali alijua mawazo yao,akasema mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu? Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayoamri duniani ya kusamehe dhambi,(amwambia yule mwenye kupooza)Ondoka,ujitwike kitanda chako,uende nyumbani kwako.Akaondoka akaenda zake nyumbani kwake.Makutano walipomwona,walishikwa na hofu,wakamtukuza Mungu,aliyewapa watu amri ya namna hii.

No comments:

Powered by Blogger.