PATA KUJUA HISTORIA YA MT.RITA KUANZIA KUZALIWA KWAKE MPAKA KIFO.

MAHALI ALIPOZALIWA.
Rita alizaliwa katika kijiji cha Roccaporena karibu na Mkoa wa Umbria huko Italia.Alizaliwa siku ya Jumamosi tarehe 22 mwezi Mei,Mwaka 1377 akiwa mtoto pekee kwa wazazi wake.kitu cha kushangaza ni kwamba alifariki dunia tarehe ileile;Jumamosi ya tarehe 22 Mwezi Mei,Mwaka 1457.Pale kijijini Roccaporena wenyeji waliona kuwa kuzaliwa kwa Rita kama mwujiza wa pekee.Hii ilitokana na ukweli kuwa umri wa mama yake Rita -Amat ulikuwa mkubwa,kiasi cha kutokuwa na matumaini ya kupata mtoto(scardo,1916;Aken,et al,1968).
Rita alibatizwa katika kanisa la Bikira Maria huko kashi.Hii ilitokana na kwamba pale Roccaporena hapakuwa na kisima cha ubatizo.Alipewa jina la Rita,jina ambalo malaika alimpa mama yake katika maono.Jina hili halikuwepo katika majina ya watakatifu kabla yake.Jina hili limekuwa maarufu tangu ubatizo wake na tokea hapo watu wengi wanapenda kuwabatiza watoto wo wa kike kwa jina hili.
Roccaporena ni kijiji kidogo maili tatu nje ya kashia,kando ya mto mdogo.Lipo bonde linalotenganisha milima na kilima kidogo na hivyo ukiangalia mandhari ya mahali pale kwa mbali utaona kama pana pia iliyosimama.Kilele cha pia,juu kabisa kuna kikanisa kimejengwa ilikutunza jiwe la Rita,mahali alipofika kusali mara kwa mara.Kuna mapokeo yanasema kuwa wakati wa kifo cha Baana weti Yesu kristo mlimani Carvari,tetemeko lilivunja mawe ya milima hii ya Roccaporena na kwamba kilima hiki jirani na kashia kilibaki kimejitenga na milima mingine.

Wazazi wake
Mwaka 1309 waliishi katika kijiji cha Roccaporena wacha Mungu,Antonio Manzini na Amata Ferri.Hawa wakikuwa wazazi wa Mt.Rita.Walikuwa wakulima wa kawaida waliotumia mali zao kuwasaidia masikini.Wanandoa hawa waliwafundisha watu kwa maneno na matendo yao namna ya kuishi kwa amani na kuwa na hofu ya Mungu.Inasemekana kuwa nyumba ya wazazi wa Mt.Rita ilikuwa hekalu ndogo la sala.Hii nikutokana na kupenda kusali na kuishi kitakatifu kadri ya amri za Mungu na za kanisa.Walipenda kutafakari mateso ya kristo asubuhi na usiku.Wote walikuwa na ibada ya pekee kwa Mama Bikira Maria.Walitoa ushauri kwa watu mbalimbali hasa wakosefu.Walijua namna bora ya kuongea na mkosefu bila kumfanya ajisikie vibaya.Kwa namna hiyo walifaulu sana kuwarudisha wengi kwa Mungu.Pamoja na kujaliwa fadhila hizi za kimungu kilichokosekana kwao ni mtoto.Mwisho Mungu aliwakirimia mtoto kama ilivyokuwa kwa Zakaria na Elizabeti.
Siku moja Amata alipokuwa akisali,malaika alimtokea katika maono akamwambia kuwa ulikuwa mpango wa Mungu kumpata mtoto msichana ambaye tangu utoto wake atakuwa ametiwa mhuri mtakatifu.Mtoto huyo atakuwa na vipawa mbalimbali na fadhila nyingi.Huyo atakuwa msaada kwa wasio na msaada kwani atakuwa mwombezi wa waliosetwa na nyota ya pekee katika kanisa.Maneno yaan malaika yalikuwa kweli kwani Amata alipata mimba na kumzaa mtoto ambaye walimwita Rita.


ISHARA ZA UTAKATIFU WA MTOTO RITA





6 comments:

  1. Naomba mwenye soft copy ya Kitabu hiki naomba msaada

    ReplyDelete
  2. Naomba kujua mwili wa mt. Ritta wa kashia bado upo kwenye basilica ya kashia..!??

    ReplyDelete
  3. Asante sana kwa kusambaza historia hii

    ReplyDelete
  4. Kupitia maombez ya mtakatifu Rita wa kashia,napokea nahitaji yangu yote niliyoomba. Amina!

    ReplyDelete
  5. Mt Rita uniombee haja za moyo wangu

    ReplyDelete

Powered by Blogger.