MASOMO YA LEO JUMAMOSI 15 JULLY,2017

Somo1:Mwa.49:29-33;50:15-25

Yakobo aliwaamuru wanawe:mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu;mnizike pamoja na baba zangu,katika pango iliyomo shambani mwa Efroni,Mhiti,katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela,iliyo mbele ya Mamre,katika nchi ya kaanani,aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti,pawe milki yake pa kuzikia.Humo walimzika Ibrahimu,na Sara mkewe;nami humo nikamzika Lea,shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa bani Hethi.Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe,akakunja miguu yake kitandani,akafa,akakisanywa pamoja na watu wake.Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa,walisema,labda Yusufu atachukia;naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda.Wakapeleka watu kwa Yusufu kunena,Baba yako alitoa amri kabla ya kufa kwake,akasema,Mwambieni Yusufu hivi,nakuomba uwaachilie ndugu zako kosa lao na dhambi yao,maana walitutenda mabaya;sasa twakuomba utuachilie kosa la watumwa wa Mungu wa baba yako.Yusufu akalia waliposema naye.Nduguze wakaenda tena,wakamwangukia miguu,wakasema,tazama,sisi tu watumwa wako.Yusufu akawaambia,msiogope.Je!Mimi ni badala ya Mungu?Nanyi kweli mlikusudia mabaya,bali Mungu aliyakusudia kuwa mema,iliitokee ili kuokoa taifa kubwa,kama ilivyo leo.Basi sasa msiogope;Mimi nitawalisha na watoto wenu.Akawafariji,na kusema nao vema.Akakaa Yusufu katika Misri,yeye na nyumba ya babaye.Akaishi Yusufu miaka mia na kumi.Yusufu akaona na wana wa Efraimu hata kizazi cha tatu;na wana wa Makiri,mwana wa Manase,walizaliwa magotini mwa Yusufu.Yusufu akawambia nduguze,Mimi ninakufa,lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka,atawapandisha kutoka nchi hii,mpaka nchi aliyowaapia Ibrahimu,na Isaka,na Yakobo.Yusufu akwaapisha wana wa Israeli,akasema,Bila shaka atawajia ninyi,nanyi mtaipandisha huko mifupa yangu.

K:Enyi mmtafutao Mungu,mioyo yenu ihuishwe.-Zab.105:1-4,6-7

Injili:Mt.10:24-33

Yesu aliwafundisha mitume:Mwanafunzi hampiti mwalimu wake,wala mtumwa hampiti bwana wake.Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake,na mtumwa kuwa kama bwana wake.Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli;je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake?Basi,msiwaogope,kwa maana hakuna neno lililositirika,ambalo halitafunuliwa;wala lililofichwa,ambalo halitajulokana.Niwaambialo ninyi katika giza,lisemeni katika nuru;na msikialo kww siri,lihubirini juu ya nyumba.Msiwaogope wauuao mwili,wasiweze kuiua roho;afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanam.Je!Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja?Wala hata mmoja haanguki chini asipojua baba yenu;lakini ninyi,hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote.Msiogope basi;bora nyinyi kuliko mashomoro wengi.Basi,kila mtu atakayenishikiri mbele ya watu,nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.Bali mtu yeyote atakaenikana mbele ya watu,nami nitamkana mbele za Baba aliyembinguni.

No comments:

Powered by Blogger.