MASOMO DOMINIKA YA 23 YA MWAKA 10 SEPTEMBA 2017

SOMO1:Eze.33:7-9

Basi wewe,mwanadamu,nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli;Basi usilisikie neno hili kinywani mwangu,ukawape maonyo yangu.Nimwambiapo mtu mbaya,Ewe mtu mbaya,hakika utakufa,nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo,aiache njia yake mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake,lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake,kusudi aiche;wala yeye asiiache;atakufa huyo katika uovu wake,lakini wewe umejiokoa roho yako.

Wimbo wa katikati Zab.95:1-2,6-9

1. Njoni tumwimbie Bwana.
Tumfanyie shangwe mwamba wa         wokovu wetu.
Tuje mbele yake kwa shukrani.

K:Ingekuwa heri leo tusikie sauti yake!Tusifanye migumu mioyo yetu.

2.Njoni,tuabudu,tusujudu,
Tupige magoti mbele za bwana aliyetuumba.
Na sisi tu watu wa malisho yake
Na sisi tu watu wa malisho yake,
Na kondoo za mkono wake.(K)

3.Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
Msiifanye migumu mioyo yenu;
Kama vile huko Meriba;
Kama siku ile ya Masa jangwani,
Hapo waliponijaribu baba zanu;.
Wakanipima,wakayaona matendo yangu.(K)

SOMO2:Rum.13:8-13

Msiwiwe na mtu chochote,isipokuwa kupendana;kwa maana ampendaye mwenzake ametimiza sheria.Maana kule kusema,Usizini,Usiue,Usiibe,Usitamani,na ikiwapo amri nyingine yoyote,inajumuishwa katika neno hili,ya kwamba,Mpende jirani yako kama nafsi yako.Pendo halimfanyii jirani neno baya,Basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.

SHANGILIO
Aleluya,Aleluya,
Mtu akinipenda,atalishika neno langu;na ana yangu atampenda;
Nasi tutakuja kwake.
 Aleluya.

INJILI:Mt.18:15-20

Siku ile Yesu aliwaambia wafuasi wake:Ndugu yako akikukosa,enenda ukamwonye,wewe na yeye peke yenu,akikusikia,umempa nduguyo.La,kama hasikii,chukua pamoja na wewe tena mtu mmoja au wawili,ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.Na asipowasikiliza wao,liambie kanisa;na asiposikiliza kanisa pia,na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.Amini,nawaambieni,yoyote mtayofunga duniani yatakuwa yamefungwa na mbinguni.Tena nawaambia,ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba,watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu ,nami nipo papo hapo katikati yao.





No comments:

Powered by Blogger.