MASOMO SIKUKUU YA MT.LAURENT,SHEMASI NA SHAHIDI ALHAMISI 10 AGOSTI 2017

SOMO1:2Kor.9:6-10

Apandaye haba atavuna haba;apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake.Si kwa huzuni wala si kwa lazima;maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa neema kwa wingi,ili ninyi mkiwa na riziki za kila namna siku zote,mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;kama ilivyoandikwa. Ametapanya,amewapa maskini,Haki yake yakaa milele. Na yeye ampaye mbegu za kupanda na kuzizidisha,naye ataongeza mazao ya haki yenu.

K:Heri atendaye fadhili na kukopesha.-Zab.112:1-2,4-,9.

INJILI:Yn.12:24-26

Yesu aliwaambia wanafunzi wake:Amini,amini,nawaambia,chembe ya ngano isipoanguka katika nchi,ikafaa,hukaa hali iyo hiyo pekee yake;bali ikifa,hutoa mazao mengi.Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza;naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele.Mtu akinitumikia,na aniguate;nami nilipo,ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo.Tena mtu akinitumikia,Baba atamheshimu.

No comments:

Powered by Blogger.