MASOMO LEO JUMATATU JUMA LA 19 LA MWAKA 14 AGOSTI 2017

SOMO1:Kum.10:12-22

Sasa,Israel,Bwana,Mungu wako,anatakaka nini kwako,ili umche Bwana,Mungu wako,na kwenda katika njia zake zote na kumpenda,na kumtumikia bwana,Mungu wako,kwa moyo wako wote,na kwa roho yako yote;kuzishika amri za Bwana na sheria zake,ninazokuamuru leo,upate uheri?Tazama,mbingu ni mali za bwana,Mungu wako,na mbingu za mbingu,na nchi na vitu vyote vilivyomo. Tena Bwana aliwafurahia baba zako,na kuwapenda na kuwachagua wazao wao baada yao,naam,na ninyi zaidi ya mataifa uote kama hivi leo.Basi zitahirini govi za mioyo yenu,wala msiwe na shingo ngumu. Kwa maana Bwana Mungu wenu,yeye ndiye Bwana wa miungu,na Bwana wa mabwana,Mungu mkuu,mwenye kuogofya,asiyependelea nyuso za watu,wala hakubali rushwa.Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki,naye humpenda mgeni,akimpa chakula na mavazi.Basi mpendeni mgeni,kwa sababu ninyi wenyewe mlikuwa wageni katika nchi ya Misri. Mche Bwana,Mungu wako,umtumikie yeye;ambatana naye,na kuapa kwa jina lake.Yeye ndiye fahari yako,na yeye ndiye Mungu wako,aliyekutendea mambo haya makubwa,yakutisha,uliyoyaona kwa macho yako. Baba zako walishukia Misri na watu sabini;na sasa Bwana,Mungu wako,amekufanya kama nyota za mbinguni kwa wingi.

K:Msifuni Bwana,ee Yerusalemu.-Zab.157:12-15,19-20.

INJILI:Mt.17:22-27

Mitume walipokuwa wakikaa Galilaya,Yesu aliwaambia,Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu,nao watamwua,na siku ya tatu atafufuka.Wakasikitika sana.Hata walipofika kapernaumu,wale watozao nusu- shekeli walimwendea Petro,wakasema,Je!Mwalimu wenu hatoi nusu-shekeli?Akasema,Hutoa.Naye alipoingia nyumbani,Yesu alitangulia kumwuliza,akisema,waonaje,Simoni?Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani?Kwa wana wao au kwa wageni?Naye aliposema,kwa wageni,Yesu alimwambia,Basi,kama ni hivyo,wana ni mahuru.Lakini tusije tukawakwaza,enenda baharini ukatupe ndoana,ukatwae samaki yule azukaye kwanza;na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli;ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako. 

No comments:

Powered by Blogger.