MASOMO YA LEO JUMATANO JUMA 19 LA MWAKA 16 AGOSTI 2017
SOMO1:Kumb.34:1-12
Musa alipanda kutoka uwanda wa Moabu mpaka mlima Nebo,hata kilele cha Pisga kukabili Yeriko.Bwana akamwonyesha nchi yote ya Galiadi hata Dani;na Naftali yote,na nchi ya Efraimu na Manase,na nchi yote ya Yuda,mpaka bahari ya magharibi;na Negebu,na uwanja wa bonde la Yeriko,mji wa mitende,hata mpaka Soari.Bwana akamwambia,Hii ndiyo nchi niliyowaapia Ibrahimu na Isaka,na Yakobo,nikisema,Nitawapa wazao wako.Basi nimekuonyesha kwa macho yako lakini hutavuka huko.Basi Musa,mtumishi wa Bwana,akafa huko,katika nchi ya Moabu,kwa neno la Bwana.Akamzika bondeni,katika nchi ya Moabu,kukabili Bethpeori;lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo.Musa alikuwa mtu wa miaka mia na ishirini alipokufa;jicho lake halikupofuka wala nguvu za mwili wake hazikupunguka.Wana wa Israeli wakamwombelezea Musa katika uwanda wa Moabu siku thelathini,basi siku za maombolezo ya matanga ya Musa zikaisha.Na Yoshua,mwana wa Nuni alikuwa amejaa ndani ya hekima;maana Musa alikuwa amemwekea mikono yake juu yake;wana wa Israeli wakamsikiliza,wakafanya kama Bwana alivyomwamuru Musa.Wala hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa,amabaye Bwana alimjua uso kwa uso;katika ishara zote na maajabu yote,ambayo Bwana alimtuma kutenda katika nchi ya Misri,kwa Farao na kwa watumishi wake wote,na nchi yake yote;na katika ule mkono wa nguvu wote,katika ule utisho mkuu wote,alioutenda Musa machoni pa Israeli wote.
K:Ahimidiwe Mungu,aliyeweka nafsi yetu katika uhai.-Zab.66:1-3,5,8,16-17
INJILI:Mt.18:15-20
Yesu aliwambia wanafunzi wake:Ndugu yako akikukosa,enenda ukamwonye,wewe na yeye peke yenu;akikusikia,umepata nduguyo.La,kama hasikii,chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili,ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.Na asipowasikiliza wao,liambie kanisa;na asiposikiliza kanisa pia,na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ishuru.Amini,nawaambieni,yoyote mtakayofunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni;na yoyote mtakayofungua duniani yatakuwa yamegunguliwa mbinguni.Tena nawaambia,ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba,watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu,nami nipo hapo katikati yao.

No comments: