MASOMO JUMA LA 18 LA MWAKA 9 AGOSTI 2017

SOMO1. Hes.13:1-2,25-14:1,26:29,34-35

Bwana alinena na Musa akamwambia tuma watu,ili waende wakaipeleleze nchi ya kaanani,niwapayo wana wa Israeli;katika kila kabila ya baba zao mtamtuma mtu mmoja,kila mtu na awe
mkuu kati yao.Wakarejea baada ya kuipeleleza nchi,mwisho wa siku arobaini.Wakaenda wakafika kwa Musa na Haruni,na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli,katika jangwa la Parani,huko kadeshi;wakawaletea Habari,wao na mkutano wote,wakawaonyesha matunda ya nchi.Wakamwambia wakasema,tulifika nchi ile uliyotutuma,na hakika yake,nchi yenye wingi wa maziwa na asali,na haya ndiyo matunda yake.Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari,na miji yao ina maboma,nayo ni makubwa sana;na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko.Amaleki anakaa karibu na nchi ya Negebu;na Mhiti,na Myebusi,na Mwamori wanakaa katika milima,na Mkanani anakaa karibu na bahari;na kando ya ukingo wa Yordani.Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa,akasema,Na tupande mara,tukaitamalaki;maana twaweza kushinda bila shaka. Bali wale watu walipopanda pamoja naye wakasema,Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa;kwa maana wana nguvu kuliko sisi.Wajawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza,wakasema,ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza,ni nchi inayo wala watu wanayoikaa;na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.Kisha,huko tuliwaona wanefili,wana wa Anaki,waliotoka kwa hao Wanefili;tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi;nao ndivyo walivyotuona sisi. Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia;watu wakatoka machozi usiku ule.Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni,na kuwaambia,Je!Nichuane na mkutano mwovu huu uninung'unikiao hata lini?Nimesikia manun'guniko ya wana wa Israeli,masikioni mwangu,ndivyo nitakavyowafanyia ninyi,mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili,na wote wliohesabiwa miongoni mwenu,kama jumla ya hesabu yenu,tangu walipopata umri wa miaka ishirini na zaidi;hao walininung'unikia.Kwa hesabu hizo siku mliyoipeleleza ile nchi,yaani,siku arobaini,kila siku kuhesabiwa mwaka,mtayachukua maovu yenu ndio miaka arobaini,nanyi mtakujua kufarikana kwangu. Mimi Bwana nmekwisha kunena,hakika yangu ndilo nitakaloutenda mkutano mwovu huu wote,waliokusanyika juu yangu;wataangamia katika nyika hii,nako ndiko watakakokufa.

K:Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!Msifanye migumu mioyo yenu.-Zan.95:1-2,6-9

INJILI:Mt.15:21-28

Yesu aliondoka Genezareti akaenda pande za Tiro na Sidoni.Na tazama,mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea,akampazia sauti akisema,Unirehemu,Bwana,Mwana wa Daudi;binti yangu amepagawa sana na pepo.Wala yeye hakumjibu neno.Nao wanafunzi wake wakamwendea,wakamwomba,wakisema,Mwache aende zake;kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.Akajibu akasema sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Naye akaja akamsujudia,akisema,Bwana unisaidie.Akajibu akasema si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.Akasema,Ndiyo,Bwana,lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.Ndipo yesu akajibu,akamwambia,Mama,imani yako ni kubwa;na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake yangu saa ile.

No comments:

Powered by Blogger.