MASOMO JUMA LA 18 LA MWAKA JUMANNE 8 AGOSTI 2017

SOMO1:Hes.12:1-13

Miriamu na Haruni walimnenea Musa kwa sababu ya mwanamke mkushi aliyekuwa amemwoa;maana,alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.Wakasema,Je! Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia?Bwana akasikia maneno yao.Basi huyo mtu,huyo Musa,alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.Bwana akanena ghafula na Musa,na Haruni,na Miriamu,na kuwaambia,tokeni nje ninyi watatu,mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje.Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa hema,akawaita Haruni na Miriamu,nao wakatoka nje wote wawili. Kisha akawaambia,sikizeni basi maneno yangu;akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu Musa;yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;kwake itanena mdomo kwa mdomo,maana,waziwazi wala si kwa mafumbo;na umbo la bwana yeye ataliona.Mbona basi ninyi hamkuogopa kumnenea mtumishi wangu,huyo Musa?Hasira za Bwana zikawa juu yao;naye akaenda zake.Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema ;na tazama Miriamu akawa mwenye ukoma,mweupe kama theluji;Haruni akamwangalia Miriamu,na tazama yu mwenye ukoma.Kisha Haruni akamwambia Musa,Ee bwana wangu,nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu,kwakuwa tumefanya upumbavu,nakufanya dhambi.Nakusihi,asiwe kama mmoja aliyekufa,ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake.Musa akamlingana Bwana,akasema,Mpoze,Ee Mungu,nakisihi sana.

K.Ee Mungu uturehemu,kwa kuwa tumetenda dhambi.-Zab.51:1-5,10-11

INJILI:Mt.14:22-36

Yesu aliwalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo,wakati yeye alipokuwa akiwaaga makutano.Naye alipokwisha kuwaaga makutano,alipanda mlima faraghani,kwenda kuomba.Na kulipokuwa jioni,alikuwako huko peke yake. Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari,kinataabika sana na mawimbi;maana upepo ulikuwa wa mbisho.Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku yesu akawaendea,akienda kwa miguu juu bahari.Wanafunzi walipomuona akienda juu ya bahari,wakafadhaika,wakisema Nikivuli;wakapiga yowe kwa hofu. Mara yesu akanena,akawaambia,jipeni moyo;ni mimi;msiogope. Petro akamjibu akasema,Bwana,ikiwa ni wewe,niamuru nije kwako juu ya maji.Akasema Njoo.Petro akashuka chomboni,akaenda akaenda kwa miguu juu ya maji,ili kumwendea yesu.Lakini alipouona upepo,akaogopa;akaanza kuzama,akapiga yowe,akisema,Bwana,niokoe.Mara yesu akanyoosha mkono wake,akamshika,akamwambia,Ewe mwenye imani haba,mbona uliona shaka?Nao walipopanda chomboni,upepo ulikoma.Nao waliokuwemo ndani ya chombo wakamsujudia,wakisema,Hakika wewe u Mwana wa Mungu.Na walipokwisha kuvuka,walifika nchi ya Genesareti.Na watu wa mahali pale walitambua,walituma watu kwenda nchi zile zilizo kandokando,wakamletea wote waliokuwa hawawezi;nao wakamsihi waguse hata pindo la vazi lake tu;na wote waliogusa wakapona kabisa.

No comments:

Powered by Blogger.