JUMAPILI DOMINIKA YA 21 YA MWAKA A 27 AGOSTI 2017.

SOMO1:Isa.22:19-23

Bwana,Bwana wa majeshi,asema hivi:Nami nitakusukuma na kukutoa katika mahali pako,naye atakushusha utoke hapa usimamapo.Na itakuwa katika siku ile nitamwita mtumishi wangu Eliakimu,mwana wa Hilkia;nami nitamvika vazi lako,nitamtia nguvu kwa mshipi wako,nami nitkabidhi yeye mamlaka yako;naye atakuwa baba kwa wenyeji wa Yerusalemu,na kwa nyumba ya Yuda.Na ufunguo wa nyumba ya Daudi nitauweka begani mwake;yeye atafungua wala hapana atakayefunga.Nami nitamkaza kama msumari mahali palipo imara;naye atakuwa kiti cha utukufu kwa nyumba ya baba yake.

Wimbo wa katikati Zab.138:1-3,6,9

1.Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,
Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu.

K:Ee Bwana,fadhili zako ni za milele Usiziache kazi za mikono yako.

2.Nitakushukuru jina lako,
Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,
Kuliko jina lako lote.
Siku ile niliyokuita uliniitikia,
Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.(k)

3.Ingawa Bwana yuko juu,amwona mnyenyekevu,
Naye amjua mwenye kijivuna tokea mbali.
Ee Bwana,fadhili zako ni za milele,
Usiziache kazi za mikono yake.(k)

SOMO2:Rum.11:33-36

Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu!Hukumu zake hazichunguziki,wali njia zake hazitafutikana!Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana?Au ni nani aliyekuwa mshauri wake?au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza,naye atalipwa tena?Kwakuwa vitu vyote vyatoka kwake,viko kwa uweza wake,tena vinarejea kwake.Utukufu una yeye milele.Amina.

INJILI:Mt.16:13-20

Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria,akawauliza wanafunzi wake akasema,Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?Wakasema,Wengine hunena Yohane Mbatizaji wengine Eliya,wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.Akawaambia,Ninyi mwaninena mimi kuwa ni nani?Simoni Petro akajibu akasema?wewe ndiyo krito,Mwana wa Mungu aliye hai.Yesu akajibu akamwambia.Heri wewe Simoni Bar-yona;kwa mwili na damu havikukufunulia hili,bali Baba yangu aliye mbinguni.Nami nakuambia,wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu;wala milango ya kizimu haitashinda.Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni;na lolote utakalo lifunga duniani,litakuwa limefunguliwa mbinguni.Ndipo alipowakataza sana wa nafunzi wake wasimwambie mtu yeyote ya kwamba yeye ndiye Kristo.

No comments:

Powered by Blogger.