MASOMO JUMA LA 20 LA MWAKA JUMAMOSI 26 AGOSTI 2017
SOMO1:Rut.2:1-3,9-11,4:13-17
Naomi alikuwa na ndugu ya mumewe,mtu mkuu mwenye mali,wa jamaa ya Elimeleki,na jina lake aliitwa Boazi.Naye Ruthu Mmoabi akamwambia Naomi,sasa niende kondeni,niokote masazo ya masuke nyuma yake yule ambaye nitaona kibali machoni pake.Akamwambia,Haya,mwanangu,Nenda.Basi akaenda,akaja akaokota masazo kondeni nyuma ya wavunaji;na bahati yake ikamtukia kwamba akaifikia sehemu ya shamba iliyokuwa mali yake huyo Boazi,ambaye alikuwa wa jamaa yake Elimeleki.Basi Boazi akamwambia Ruthu,Mwanangu,sikiliza;hapa karibu na wasichana wangu.Macho yako na yaelekee konde walivunalo,ufuatane nao,Je!Sikuwaagiza vijana wasikuguse?Tena,Ukiona kiu,uende kwenye vyombo,nawe uyanywe waliyoyateka hao vijana.Ndipo aliposujudia,akainama mpaka nchi,akamwambia,Jinsi gani nimepata kibali machoni pako,hata ukanifahamu,mimi niliye mgeni?Naye Boazi akajibu,akamwambia,Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo,tangu alipokufa mumeo;na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako,na nchi yako uliyozaliwa,ukawafikilia watu usiowajua tangu hapo.Basi Boazi akamtwaa Ruthu,naye akawa mke wake;naye akaingia kwake;na Bwana akamjalia kuchukua Mimba,naye akazaa mtoto wa kiume.Nao wali wanawake wakamwambia Naomi,na ahimidiwe Bwana,asiyekuacha leo hali huna jamaa aliyekaribu;jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli.Naye atakurejeza uhai wako na kukuangalia katika uzee wako;kwa maana mkweo,ambaye akupenda,naye anakufaa kuliko watoto saba,ndiye aliyemzaa.Basi Naomi akamtwaa yule mtoto,akamweka kifuani pake,akawa mlezi wake.Nao wale wanawake waliokuwa jirani zake wakampa jina,wakisema,Naomi amezaliwa mwana;wakamwita jina lake Obedi;yeye ndiye baba yake Yese,aliye baba yake Daudi.
K:Tazama,atabarikiwa hivyo,yule amchaye Bwana.-Zab.128:1-5
INJILI:Mt.23:1-12
Yesu aliwaambia makutano na wanafunzi wake,akasema,Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa;basi,yoyote watakayowaambia,myashike,na kuyatenda,lakini kwa mfano wa matendo yao,msitende;maana wao hunena lakini hawatendi.Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao;wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao.Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu;kwa kuwa hupanua hirizi zao,huongeza matamvua yao;hupenda viti vya mbele katika karamu,na kuketi mbele katika masinagogi,na kusalimiwa masokoni,na kuitwa na watu,Rabi.Bali ninyi msiitwe Rabi,maana mwalimu wenu ni mmoja,aliye wambinguni.Wala msiitwe viongozi;maana kiongozi wenu ni mmoja,naye ndiye kristo.Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu.Na yeyote atakayejikweza,atadhiliwa;na yeyote atakayejidhili,atakwezwa.

No comments: