MASOMO JUMA LA 20 LA MWAKA LEO IJUMAA 25 AGOSTI 2017
SOMO1:Rut.1:1,3-6,14-16,22.
Ikawa zamani za waamuzi walipoamua,kulikuwa na njaa katika nchi. Akaondoka mtu mmoja wa Bathlehemu ya Yuda akaenda kukaa katika nchi ya ya Moabu,yeye na mkewe na wanawe wawili.Akafa Elimeleki,mumewe Naomi;na yule mwanamke akasalia na wanawe wawili.Nao wakaoa wake katika wanawake wa Moabu;na jina la mmoja aliitwa Orpa,na jina la wapili Ruthu.Wakakaa huko yapata miaka kumi.Wakafa na Maloni na kilioni wote wawili,na mumewe pia.Ndipo alipoondoka,yeye na wakweze,ili kurudi kutoka nchi ya Moabu;maana huko katika nchi ya Moanu amesikia ya kwamba Bwana amewajilia watu wake na kuwapa chakula.Orpa akambusu mkwewe,akarejea kwa watu wake,lakini Ruthu akaambatana naye.Naye akasema,tazama,shemeji yako amerejea kwa watu wake,na kwa Mungu wake;basi urejee wewe umfuate shemeji yako.Naye Ruthu akasema,usinisihi nikuache,nirejee nisifuatane nawe;maana wewe uendako nitakwenda,na wewe ukaapo nitakaa.Watu wako watakuwa watu wangu,na Mungu wako atakuwa Mungu wangu.Basi Naomi akarudi;pamoja na Ruthu Mmoabu,mkwewe;ambao walirudi mwanzo wa mavuno ya shayiri.
K:Ee nafsi yangu,umsifu Bwana.-Zab 146:5-10
INJILI:Mt.22:34-40
Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo,walifanya shauri pamoja.Mmoja wao,mwana-sheri,akamwuliza,akimjaribu;Mwalimu,katika torati ni amri ipi iliyo kuu?Akamwambia,Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,na kwa roho yako yote,na kwa akili zako zote.Hii ndiyo amri iliyo kuu,tena ya kwanza.Na ya pili yafanana nayo,ni hii,Mpende jirani yako kama nafsi yako.Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.

No comments: