MASOMO JUMATATU JUMA LA 21 LA MWAKA 28 AGOSTI 2017
SOMO 1:1The.1:2-5,9-10
Twamshukuru Mungu siku zote kwaajili yenu nyote,tukiwataja katika maombi yetu.Wala hatuachi kuikumbuka kazi ya Imani,na taabu yenu ya upendo,na saburi yenu ya tumaini lililo katika bwana wetu yesu kristu,mbele za Mungu Baba yetu.
Kwa maana,ndugu mnapopendwa na Mungu twajua uteule wenu;ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu bali katika nguvu,na katika Roho mtakatifu,na uthibiti mwingi;kama vile mnavyojua jinsi zitakavyokuwa tabia zetu kwenu,kwa ajili yenu.
Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma,si katika Makedonia na Akaya tu,ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea;hata hatuna haja sisi kunena lolote.Kwakuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu,jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu;na jinsi mlivyogeukia Mungu aliye hai,wa kweli;na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni,ambaye alimfufua katika wafu,naye ni Yesu,mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayo kuja.
K:Bwana awaridhia watu wake.-Zab.149:1-6
INJILI:Mt.23:13-22
Yesu aliwaambia makutano na wafuasi wake:Ole wenu waandishi na Mafarisayo,wanafiki!Kwakuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni;ninyi wenyewe hamuuingii,wala wanaoingia hamwaachi waingie.Ole wenu waandishi na Mafarisayo,wanafiki!Kwakuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofuna akiisha kufanyika,mnamfanya kuwa mwana wa jehanu mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.Ole wenu viongozi vipofu,ninyi msemao,Mtu atakayeapa kwa hekalu,si kitu,bali mtu atakayeapa kwa dhahabu ya hekalu amejifunga.Wapumbavu ninyi na vipofu;maana ni ipi iliyokubwa,ile dhahabu,au ile hekalu liitakasayo dhahabu?Tena mtu atakayeapa kwa madhabahu,si kitu;bali atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake,amejifunga.Vipofu ninyi;maana ni ipi iliyo kubwa,ile sadaka,au ile madhabahu iitakasayo sadaka?Basi yeye aapaye kwa madhabahu,huapa kwa hiyo,na kwa vitu vyote vilivyo juu yake.Naye aapaye kwa hekalu,huapa kwa hilo,na kwa yeye akaaye ndani yake .Naye aapaye kwa mbingu,huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu,na kwa yeye aketiye juu yake.

No comments: