MASOMO YA MISA NOVEMBA 6 DECEMBA 2017 JUMA LA 31 LA MWAKA

SOMO 1:Rum.11.29-36

Karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake.
Kwa maana kama ninyi zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepta rehema kwa kuasi kwao; kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema. Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena? Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 69:29-30, 32-33, 35-36 (K) 14

(K) Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Ee Bwana.

Nami niliye maskini na mtu wa huzuni.
Mungu, wokovu wako utaniinua.
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,
Nami nitamtukuza kwa shukrani. (K)

Walioonewa watakapoona watafurahi;
Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.
Kwa kuwa Bwana huwasikia wahitaji,
Wala hawadharau wafunga wake. (K)

Maana Mungu ataiokoa Sayuni,
Na kuijenga miji ya Yuda,
Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki.
Wazao wa watumishi wake watairithi,
Nao walipendao jina lake watakaa humo. (K)

SHANGILIO
Zab. 119:105

Aleluya, aleluya,
Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.

INJILI:Lk.14:12-14


Yesu alimwambia yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.

No comments:

Powered by Blogger.