SIKUKUU YA KUTUKUKA KWA MSALABA ALHAMISI 14 SEPTEMBA 2017

SOMO1:Hes.21:4-9

Siku zile jangwani watu walimnung'unikia Mungu na Musa,Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri,ili tufe jangwani?Maana hapana chakula,wala hapana maji,na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu.Bwana akatuma Nyoka za moto kati ya watu wakawauma,watu wengi wakafa.Watu wakamwendea Musa wakasema,Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu na wewe;utuombee kwa Bwana atuondolee nyoka hawa.Basi Musa akawaombea watu.Bwana akamwambia Musa,jifanyie nyoka ya shaba,ukaiweke juu ya mti,na itakuwa kila mtu aliyeumwa,aitazamapo,ataishi.Musa akafanya nyoka ya shaba,akaiweka juu ya mti,hata ikiwa nyoka amemwuma mtu,alipoitazama ile nyoka ya shaba,akaishi.

K:Msiyasahau matendo ya Mungu.-Zab.78:1-2,34-38


SOMO2:Fil.2:6-11

Yesu Kristo alikuwa yuna namna ya Mungu,naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;bali alijifanya kuwa hana utukufu,akatwaa namna ya mtumwa,akawa na mfano wa wanadamu;tena alipoonekana ana umbo kama mwanadamu,alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti,naam,mauti ya msalaba.Kwahiyo tena Mungu alimwadhimisha mno,akamkirimia jina lile lipitalo kila jina,ili kwa jina la Yesu kila hoti lipigwe,la vitu vya mbinguni,na vya dunia,chini ya nchi;na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana,kwa utukufu wa Mungu Baba.

INJILI:Yn.3:13-17

Yesu alimwambia Nikodemu:Hakuna aliyepaa mbinguni,ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni,yaani Mwana wa Adamu.Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa mwanawe wa  pekee,ili kila mtu amwaminiye asipotee,bali awe na uzima wa milele.Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu,bali ulimwengu uokolewe katika yeye.

No comments:

Powered by Blogger.