JUMA LA 23 LA MWAKA 15 SEPTEMBA 2017

SOMO1:1Tim.1:1-2,12-14

Paulo,mtume wa Kristo Yesu,kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na Kristo Yesu,taraja letu;kwa Timotheo,mwanangu hasa katika imani.Neema na iwe kwako,na rehema,na amani,zitokazo kwa Mungu Baba na Kwa Kristo Yesu Bwana wetu.Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu,akaniweka katika utumishi wake;ingawa hapo kwanza nalikuwa mtukanaji,mwenye kuudhi watu,mwenye jeuri;lakini nalipata rehema kwa kuwa nilitenda hivyo kwa ujinga,na kwa kutokuwa na imani.Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na upendo lililo katika kristo Yesu.

K:Bwana ndiye fungu la posho langu.-Zab.16:1-2,5,7-8,11.

INJILI:Lk.6:39-42

Yesu aliwaambia wanafunzi wake mithali,Je! Aliye kipofu aweza kuongoza kipofu? Hawatatumbukia shimoni wote wawili?Mwanafunzi hawi mkuu kuliko mwalimu wake,lakini kila mtu ambaye amehitimu hulingana na mwalimu wake.Basi,mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako,na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?Au,utawezaje kumwambia ndugu yako,Ndugu yangu,niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako,nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe?Mnafiki wewe,itoe kwanza boriti katika jicho lako mwenyewe,ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako.

No comments:

Powered by Blogger.