MASOMO JUMA LA 23 LA MWAKA 16 SEPTEMBA 2017
SOMO1:1Tim.1:15-17
Ni neno la kuaminiwa,tena lastahili kukubalika kabisa,ya kwamba kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi;ambao wakwanza wao ni mimi.Lakini kwaajili hii nalipata rehema,ili katika mimi wa kwanza,Yesu kristo audhihirishe uvumilivu wake wote;niwe kielelezo kwa wale watakao mwamini baadaye,wapate uzima wa milele.Sasa kwa ufalme wa milele asiyeweza kuona uharibifu,asiyeonekana,Mungu peke yake,na iwe heshima na utukufu milele na milele.Amina.
K:Jina la Bwana lihimidiwe tangu leo na hata milele.-Zab.113:1-7
INJILI:Lk.6:43-49
Yesu aliwaambia wanafunzi wake:Hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya,wala mti mbaya uzaao matunda mazuri;kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake;maana,katika miiba hawachumi tini,wala katika michongoma hawachumi zabibu.Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema,na mti mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu;kwa kuwa mtu,kinywa chake hunena yale yaujazao moyo wake.Na kwa nini mnaniita,Bwana,walakini hamyatendi nisemayo? Kila mtu ajaye kwangu,na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda,nitawaonyesha.Mfano wake wake ni mtu ajengaye nyumba,na kuchimba chini sana,na kuweka msingi juu ya mwamba,na kulipokuja gharika,mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu,usiweze kiitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.Lakini yule aliyesikia ila hakutenda,mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi,mto ukaishukia kwa nguvu,ikaanguka mara;na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa.

No comments: