MASOMO SIKUKUU YA MT.MIKAELI,GABTIELI NA RAFAEL,MALAIKA WAKUU WAKUU IJUMAA 29 SEPTEMBA 2017
SOMO 1:Dan.7:9-10,13-14
Nilitazama viti vya enzi vikawekwa,na mmoja aliye mzee wa siku ameketi;mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji,na nywele za kichwa chake kama sufu safi;kiti chake cha enzi kilikua na miali ya moto,na gurudumu za moto uwakao.Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake;maelfu-elfu wakamtumikia,na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake;hukumu ikawekwa,na vitabu vikafunuliwa.Nikaona katika njozi za usiku,na tazama,mmoja aliyemfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku,wakamleta karibu naye.Naye akapewa mamlaka,na utukufu,na ufalme,ili watu wa kabila zote,na taifa zote,na lugha zote,wamtumikie;mamlaka yake ni ya milele,ambayo haitapita kamwe,na ufalme wake ni ufalme isioweza kuangamizwa.
K:Mbele ya Miungu nitakuimbia Zaburi.-Zab.138:1-5
INJILI:Yn.1:47-51
Yesu alipomwona Nathanaeli anakuja kwake,akanena habari zake,Tazama,Mwisraeli kwelikweli,hamna hila ndani yake.Nathanaeli akamwambia,Umepataje kunitambua?Yesu akajibu,akamwambia,kabla Filipo hajakuita,ulipokuwa chini ya mtini nilikuona.Nathanaeli akamjibu,Rabi,wewe u Mwana wa Mungu,ndiwe mfalme wa Israeli.Yesu akajibu,akamwambia,kwa sababu nilikuambia,nilikuambia nilikuona chini ya mtini,waamini?Utaona mambo makubwa kuliko haya.Akamwambia,Amin,amin,nawaambia,Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.

No comments: