MASOMO JUMA LA 25 LA MWAKA JUMAMOSI 30 SEPTEMBA 2017

SOMO 1:Zek.2:1-5,10-11

Niliinua macho yangu,nikaona,natazama,mtu mwenye kamba ya kupimia mkoni mwake .Ndipo nikasema,unakwenda wapi?Akaniambia ,ninakwenda kuupima Yerusalemu,nione upana wake ulivyo na ulivyo na urefu wake ulivyo .Na tazama ,yule malaika aliyesema nami akasimama karibu ,na malaika mwingine akatoka ili kuonana naye ;naye akamwambia ,piga mbio,kamwambie kijana huyu ,na kusema ,Yerusalemu utakaliwà na watu ,kama vijiji visivyo na kuta ,kwa sababu ya wingi  wa watu na mifugo iliyomo ndani yake.Kwa maana mimi ,asema Bwana ,nitakuwa ukuta wa moto  kuuzunguka pande zote,nami nutakuwa huo utukufu ndani yake .imba,ufurahi,Ee binti Sayuni ;maana tazama,nitakuja ,nami nitakaa,kati yako,asema Bwana.na Mataifa mengi watajiunga na bwana katika siku ile ,nao watakua watu wangu.


K:Bwana atatulinda kama mchungaji alindavyo kundi lake-Yer.31:10-13

INJILI:Lk.9:43-45


Makutano walipo kua wakiyastaajabia mambo yote aliyoyafanya,Yesu aliwaambia  wanafunzi wake ,yashikeni maneno haya masikioni mwenu,kwakuwa mwana wa Adamu anakwenda  kutiwa katika mikono ya watu.Lakini hawakulifahamu neno lile,likafichwa kwao  wasilitambue;wakaogopa kumwuliza maana ya neno lile.

No comments:

Powered by Blogger.