MASOMO JUMA LA 25 LA MWAKA ALHAMISI 28 SEPTEMBA 2017
Katika mwaka wa pili wa Dario mfalme,mwezi,wa sita,siku ya kwanza ya mwezi,neno la Bwana lilimjia Zerubabeli,mwana wa Shealtieli,liwali wa Yuda na Yoshua,mwana wa Yeosadaki,kuhani mkuu,kwa kinywa chake Hagai nabii,kusema,Bwana wa Majeshi asema hivi ya kwamba,watu hawa husema,hu sio wakati upasao kuja,huu sio wakati wa kujengwa nyumba ya Bwana.Ndipo neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai,kusema,Je! Huu ndio wakati nanyi kukaa katika nyumba ya zenye mapambo ya mbao,iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika? Basi sasa.Bwana wa majeshi asema hivi,Zitafakarini njia zenu.Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo;mnakula,mnakunywa lakini hamkujazwa na mfuko uliotoboka-toboka.Bwana wa majeshi asema hivi,Zitafakarini njia zenu.Pandeni milimani,mkalete miti,mkaijenge nyumba;nami nitaifurahia,nami nitatukuzw,asema Bwana.
K:Bwana awaridhia watu wake.-Zab.149:1-6,9
INJILI:LK.9:7-9
Herode mfalme alisikia habari za yote yaliyotendeka akafadhaika kwa sababu watu wengine walisema ya kwamba Yohane amefufuka katika wafu,na wengine ya kwamba Eliya ametokea,na wengine ya kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.Lakini Herode akasema,Yohane nilimkata kichwa;basi ni nani huyu ambaye ninasikia mambo haya juu yake? Akataka kumwona.
No comments: