MASOMO SIKUKUU YA MT.MATHAYO MTUME NA MWINJILI ALHAMISI 21 SEPTEMBA 2017

SOMO 1:Efe.4:1-7,11-13

Nawasihi mimi niliye mfungwa katika Bwana,mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;kwa unyenyekevu wote,na upole,kwa uvumilivu,mkichukuliana katika Upendo;nakujitahidi kuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.Mwili mmoja,na Roho mmoja,kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.Bwana mmoja,imani moja,ubatizo mmoja.Mungu mmoja naye ni Baba wa wote,aliye juu ya yote na katika yote,na ndani ya yote.Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.Naye alitoa wengine kuwa mitume;na mwingine kuwa manabii;na wengine kuwa wainjilisti;na wengine kuwa wachungaji na waalimu;kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu,hata kazi ya huduma itende,hata mwili wa Kristo ujengewe;hata sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kufahamu sana Mwana  wa Mungu,hata kuwa mtu mkamilifu,hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo.

K:Sauti yao imeenea duniani mwote.-Zab.19:1-4

INJILI:Mt.9:9-13

Yesu alipokuwa akipita aliona mtu ameketi forodhani,aitwaye Mathayo,akamwambia,Nifuate.Akaondoka,akamfuata.Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula,tazama,watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake.Mafarisayo walipoona,waliwaambia wanafunzi wake,Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?Naye aliposikia,aliwaambia,wenye afya hawaitaji tabibu,bali walio hawawezi.Lakini nendeni,mkajifunze maana yake maneno haya,Nataka rehema,wala si sadaka;kwa maana sikuja kuwaita wenye haki,bali wenye dhambi.


No comments:

Powered by Blogger.