MASOMO JUMA LA 24 LA MWAKA JUMANNE 19 SEPTEMBA 2017
SOMO 1:1Tim.3:1-13
Ni neno la kuaminiwa;mtu akitaka kazi ya askofu,atamani kazi njema.Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika,mume wa mke mmoja,mwenye kiasi na busara,mtu wa ustaarabu,mkaribishaji,ajuaye kufundisha;si mtu wa kizoelea ulevi,si mpiga watu;bali awe mpole;si mtu wa kujadiliana,wala asiwe mtu wa kupenda fedha;mwenye kuisimamia nyumba yake vema,ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;(yaani mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe,alitunzaye kanisa la Mungu?) wala asiwe mtu aliyeongoka karibu,asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu wa nje;ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu;si wenye kauli mbili,si watu wa kutumia mvinyi sana,si watu wenye kauli mbili,si watu wenye kutumia mvinyo sana,si watu wanaotamani fedha ya aibu;waishike siri ya imani katika dhamira safi.Hawa pia na wajaribiwe kwanza;baadaye waitende kazi ya shemasi wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia.Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu;si wasingiziaji;watu wa kiasi,waaminifu katika mambo yote.Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja,wakisimamia watoto wao vizuri,na nyumba zao.Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja zuri,na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.
K:Nitakwenda kwa unyofu wa moyo.-Zab:101:1-3,5,6.
INJILI:Lk.7:11-17
Yesu alikwenda mpaka mji mmoja uitwao Naini,wanafunzi wake walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa.Na alipokaribia lango la mji,hapo palikua na maiti anachukuliwa nje,ni mwana wa pekee wa mamaye ambaye ni mjane,na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye.Bwana alipomwona alimwonea huruma,akamwambia,usilie.Akakaribia,akaligusa geneza;wale walio kuwa wakilichukua wakasimama.Akasema,Kijana,nakuambia,Inuka.Yule maiti akainuka,akaketi akaanza kusema.Akampa mama yake.Hofu ikawashika wote,Wakamtukuza Mungu,wakisema,Nabii mkuu ametokea kwetu;na,Mungu amewaangalia watu wake.habari hii yake ikaenea katika Uyahudi wote,na katika nchi zote za kando kando.

No comments: