MASOMO DOMINIKA YA 22 YA MWAKA 3 SEPTEMBA 2017
SOMO1:Yer.20:7-9
Ee Bwana,umenihadaa,nami nimehadaika;wewe una nguvu kuliko mimi,ukashinda;nimekuwa kitu cha kuchekesha,mchana kutwa;kila mtu hunidhihaki.Maana kila ninenapo napiga kelele;nalia,Dhuluma na uharibifu!Kwakuwa neno la Bwana limefanywa shutumu kwangu,na dhihaka,mchana kutwa.Nami nikisema,Sitamtaja wala sitasema tena kwa jina lake;ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao,uliofungwa ndani ya mifupa yangu,nami nimechoka kwa kustahimili,wala siwezi kujizuia.
Wimbo wa katikati Zab.63:1-5,7-8
1.Ee Mungu,Mungu wangu,nitakutafuta mapema,
Nafsi yangu inakuonea kiu.
Mwili wangu wakuonea shauku,
Katika nchi kame na chovu,isiyo na maji.
K:Ee Bwana,Mungu wangu,Nafsi yangu inakuonea kiu.
2.Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu,
Nizione nguvu zako na utukufu wako.
Maana fadhili zako njema kuliko uhai,
Midomo yangu itakisifu.(K)
3.Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai,
Kwa jina lako nitainua mikono yangu.
Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono,
Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.(K)
4.Maana wewe umekuwa msaada wangu,
Na uvulini mwa mbawa zako nitashangulia.
Nafsi yangu imekuaandama sana,
Mkono wako wa kuume unanitegemeza.(K)
SOMO2:Rum.12:1-2
Basi,ndugu zangu,nawasihi,kwa huruma zake Mungu itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai,takatifu,ya kumpendeza Mungu,ndiyo ibada yenu yenye maana.Wala msifuatishe namna ya dunia hii;bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu,mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema,ya kumpendeza,na ukamilifu.
SHANGILIO Lk.21:36
Aleluya,aleluya
Kesheni ninyi kila wakati,ili mpate kuokoka
Na kusimama mbele ya Mwana wa Adamu.
Aleluya.
INJILI:Mt.16:21-27
Tangu wakati huo Yesu aliaanza kuwaonya wanafunzi wake ua kwamba imempasa kwenda Yerusalemu,na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makihani,na waandishi,na kuuawa,na siku ya tatu kufufuka.Petro akamchukua akaanza kumkemea,akisema Hasha,Bwana hayo hayatakupata.Akageuka,akamwambia Petro,Nenda nyuma yangu,Shetani;u kikwazo kwangu;maana huyawazi yaliyo ya Mungu,bali ya wanadamu.
Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake,Mtu yeyote akitaka kunifuata,na ajikane mwenyewe,ajitwike msalaba wake,anifuate.Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake,ataipoteza;na mtu atakayepoteza nafsi yake kwaajili yangu,ataiona.Kwani atafikiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote,na kupata hasara ya nafsi yake?Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba
yake pamoja na malaika zake;ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

No comments: