MASOMO JUMATANO JUMA LA 21 LA MWAKA 30 AGOSTI 2017
SOMO1:1The.2:9-13
Ndugu mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu;kwakuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote,tukawahubiri hivi injili ya Mungu.Ninyi ni mashahidi,na Mungu pia,jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini,kwa utakatifu na kwa haki,bila kulaumiwa;vilevile,kama mjuavyo,jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe,tukiwatia moyo na kushuhudia ili mwenende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu,mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.Kwasababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma,kwa kuwa,mlipopata lile neno la Mungu mliolisikia kwetu,mliolipokea si kama neno la wanadamu,bali kama neno la Mungu;na ndivyo lilivyo kwelikweli;litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.
K:Ee Bwana umenichunguza na kunijua.-Zab.139:7-12
INJILI:Mt.23:27-32
Yesu alisema,Ole wenu,waandishi na Mafarisayo,wanafiki!kwa kuwa mmefanana na makaburi yalipakwa chokaa nje yaonekana kuwa mazuri,bali ndani yamejaa mifupa ya wafu na uchafu wote.Vivyo hivyo ninyi nanyi,kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki,bali ndani mmejaa unafiki na maasi.Ole wenu,waandishi na Mafarisayo,wanafiki! kwakuwa mnayajenga makaburi ya manabii,na kuyapamba maziara ya wenye haki,na kusema,kama sisi tungalikuwapo zamani za baba zetu,hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii.Hivi mwajishuhudia wenyewe,ya kwamba ninyi ni wana wao waliouawa manabii.Kijazeni basi kipimo cha baba ze

No comments: