JUMA LA 21 LA MWAKA KUMBUKUMBU YA KUFA SHAHIDI MT.YOHANE MBATIZAJI 29 AGOSTI 2017

SOMO1:1The.2:1-8

Ninyi wenyewe,ndugu,mwakujua kuingia kwetu kwenu,ya kwamba hakukuwa bure;lakini tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri,kama mjuavyo,katika filipi,twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu,kwa kuishindania sana.Kwa maana maonyo yetu sio ya ukosefu,wala ya uchafu,wala ya hila;bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuweke amana Injili,ndivyo tunenavyo;si kama wapendezao Mungu anayetupima mioyo yetu.Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wowote,kama mjuavyo,wala maneno ya juu juu ya kuficha choyo;Mungu ni shahidi.Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu,wala kwenu wala kwa wengine tulipokuwa tukiweza kuwalemea kama mitume wa kristo;bali tulikuwa wapole katikati yenu,kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe.Vivyo hivyo nasi tukiwatumaini kwa upendo mwingi,tuliona furaha kuwapa,si Injili ya Mungu tu,bali na roho zetu pia,kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.

K:Ee Bwana umenichunguza na kunijua.-Zab.138:1-3,4-6

INJILI:Mt.23:23-26

Yesu alisema,Ole wenu waandishi na Mafarisayo,wanafiki!kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira,lakini mmeacha mambo makuu ya sheria,yaani,adili,na rehema,na imani;hayo imewapasa kuyafanya,wala yale mengine msiyaache.Viongozi vipofu,wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.Ole wenu Waandishi na Mafarisayo,wanafiki! Kwakuwa mnasafisha nje ya kikombe na cha chano,na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi.Ewe Farisayo kipofu,safisha kwanza ndani ya kikombe,ili nje yake nayo ipate kuwa safi.

No comments:

Powered by Blogger.