MASOMO JUMA LA 22 LA MWAKA 6 SEPTEMBA 2017

SOMO1:Kol.1:1-8

Paulo,mtume wa kristu Yesu kwa mapenzi ya Mungu,na Timotheo ndugu yetu,kwa ndugu watakatifu,waaminifu katika kristo,walioko Kolosai.Neema na iwe kwenu,na amani zitokazo kwa Mungu,Baba yake Bwana wetu yesu kristo,siku zote tukiwaombea;tangu tusiposikia habari za imani yenu katika kristo Yesu,na upendo mlio nao kwa watakatifu wote;kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni;ambalo habari zake mlizisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili;iliyofika kwenu,kama ilivyo katika ulimwengu wote,na kuzaa matunda na kukua,kama inavyokuwa kwenu pia,tangu siku mlipoisikia mkaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli;kama mlivyofundishwa na Epafra,mjoli wetu mpenzi,aliye mhudumu mwaminifu wa kristo kwa ajili yenu;naye alitueleza upendo wenu katika Roho.

K:Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.-Zab.52:8-9

INJILI:Lk.4:38-44

Yesu alitoka katika sinagogi,akaingia katika nyumba ya Simoni.Naye mkwewe Simoni,mamaye mkewe,alikuwa ameshikwa na homa kali,wakamwomba kwa ajili yake.Akasimama karibu naye,akaikemea ile homa,ikamwacha;mara hiyo akaondoka,akawatumikia.Na jua lilipokuwa likichwa,wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbalimbali waliwaleta kwake,akaweka mikono yake juu ya kila mmoja akawaponya.Pepo nao waliwatoka watu wengi,wakipiga kelele na kusema,Wewe u mwana wa Mungu.Akawakemea,asiwaache kunena,kws sababu walimjua kuwa ndiye kristo.Hata kulipokucha alitoka akaenda mahali pasipokuwa na watu;makutano wakawa wakimtafuta-tafuta,wakafika kwake,wakataka kumzuia asiondoke kwao.Akawaambia,Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia;maana kwa sababu hiyo nalitumwa.Basi,alikuwa akihubiri katika masinagogi ya Galilaya.

No comments:

Powered by Blogger.