MASOMO YA LEO JUMATATU JUMA LA 20 LA MWAKA 21 AGOSTI 2017

SOMO1:Amu.2:11-19

Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana,nao wakawatumikia Mabaali Wakamwacha Bwana. Mungu wa baba zao,aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri,wakafuata miungu mingine,baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote,wakajinamisha mbele yao;wakamkasirisha Bwana,akaghadhabika . Wakamwacha Bwana,wakaitumikia Baali na Mashtorethi.Hasira ya Bwana ikawa juu ya Israeli,naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara,akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote;hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.Kila waliokwenda,mkono wa Bwana ulikuwa juu ya kuwatenda mabaya,kama Bwana alivyosema,na kama bwana  alivyowaapia;nao wakafadhaika sana.Kisha bwana akawainua waamuzi,waliowaokoa na mikono ya watu hao waliowateka waliowaokoa na mikono ya watu hao walio wateka,nyara.Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi,maana walifanya uasherati kwa kiifuata miungu mingine,wakajiinamisha mbele yao;Wakageuka upesi,na kuicha njia ile walioitendea waamuzi,ndipo Bwana alikuwa pamoja na mwamuzi huyo,akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo;maana Bwana alighairi kwa ajili ya kuugua kwao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua.Lakini ikawa,wakati alipokufa mwamuzi huyo,wakarudi nyuma wakafanya maovu kuliko baba zao,kwa kuifuata miungu mingine ili kuitumikia,na kuinama mbele;hawakuacha matendo yao,wala njia zao za ukaidi.

K:Ee Bwana unikumbuke mimi,kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.-Zab.106:34-37,39-40,43-44.

INJILI:Mt.19:16-22

Mtu mmoja alimwendea yesu akamwambia,Mwalimu,nitende jambo gani jema,ili nipate uzima wa milele?Akawaambia,kwani nkujiuliza habati ya wema?Aliye mwema ni mmoja.Lakini ukitaka kuingia katika uzima,zishike amri. Akamwambia zipi?Yesu akasema,Ni hizi,Usiue,Usizini,Usishuhudie uongo,Waheshimu baba yako na mama yako na mpende jirani yako kama nafsi yako. Yule kijana akamwambia,Haya yote nimeyashika,nimepungukiwa nini tena?Yesu akamwambia,Ukitaka kuwa mkamilifu,enenda ukauze ulivyo navyo,uwape maskini,nawe utakuwa na hazina mbinguni;kisha njoo unifuate.Yule kijana aliposikia neno lile,akaenda zake kwa huzuni;kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

No comments:

Powered by Blogger.