MASOMO YA LEO JUMANNE JUMA LA 20 LA MWAKA 22 AGOSTI 2017
SOMO1:Amu.6:11-24
Malaika wa Bwana alienda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra,uliokuwa mali yake Yoashi,Mwabiezeri;na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo,ili kuficha machoni pa Wamidiani.Malaika wa bwana akamtokea,akamwambia,Bwana yu pamoja nawe,Ee shujaa. Gideoni akamwambia,Ee Bwana wangu,ikiwa bwana yu pamoja nasi na mbona mambo haya yote yametupata?Yako wapi matendo yake ya ajabu,waliotuhafithia babu zetu,wakisema,Je!Siye bwana aliyetuleta huku kutoka Misri?Ila sasa ametutupa,naye ametutia katika mikono ya Midiani.Bwana akamtazama,akasema,enenda kwa uwezo wako huu,ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma?Akamwambia,Ee Bwana,nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani?Tazama,jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase,na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu. Bwana akamwambia,hakika nitakuwa nawe,nawe utawapiga Wamiadini kama mtu mmoja.Naye akamwambia,kama nimepata kibali mbele za macho yako,basi unionyeshe ishara,ya kuwa ndiwe wewe unayesema nami.Tafadhali usiondoke hapa hata nikujue,nikatoe zawadi yangu,na kuiweka mbele zako.Akasema,Nitangoja hata utakaporudi.Basi Gideoni akainhia ndani,akaanda mwna-mbuzi ,na mikate isiyotiwa chachu,ya efa ya unga;akaitia ile nyama katika kikapu,akautia mchuzi katika Nyungu,akamletea hapo nje chini ya mwaloni,akampa.Naye Malaika wa Mungu akamwambia,itwae nyama na mikate isiyotiwa chachu uiweke juu ya mwamba huu,ukaumwage huu mchuzi. Akafanya hivyo. Ndipo malaika wa bwana akanyosha ncha ya fimbo ile iliyokuwa mkononi mwake,akaigusa ile nyama na mikate;malaika wa bwana akaondoka mbele ya macho yake . Gideoni akaona ya kuwa ni malaika wa bwana. Gideoni akasema,Ole wangu,Ee Bwana Mungu!kwa kuwa nimemwona Bwana uso kwa uso . Bwana,akamwambia,Amani iwe pamoja nawe;usiogope hutakufa.Ndipo Gideoni akamjengea bwana madhabahu hapo,akaita jina lake,Yehova shalomu;hata hivi leo iko huko Ofra ya Waabiezeri.
K:Bwana atawambia watu wake amani.-Zab.85:8,10-13
INJILI:Mt.19:23-30
Yesu aliwambia Wanafunzi wake,Amini,nawaambieni,ya kwamba itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. Nawambia tena,ni rahisi zaidi kwa Ngamia kupenya tundu la sindano,kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Wanafunzi wasiposikia,walishangaa mno,wakisema,Ni nani basi awezaye kuokoka?Yesu akawakazia macho,akawambia,kwa mwanadamu hilo haliwezekani;bali kwa Mungu yote yawezekana.Ndipo Petro akajibu,akamwambia,Tazama,sisis tumeacha vyote tukakufuata;tutapata nini basi?Yesu akawambia,Amini,nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi,katika ulimwengu mpya,atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake,ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili,mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli. Na kila mtu aliyeacha nyumba,au ndugu wa kiume au wa kike,au baba,au mama,au watoto au mashamba,kwaajili ya jina langu,atapokea mara mia,na kuurithi uzima wa milele. Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho,na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.

No comments: