JUMAPILI DOMINIKA YA 20 YQ MWAKA(Mwaka A) 20 AGOSTI 2017
SOMO1:Isa.56:1,6-7
Bwana asema hivi,Shikeni hukumu,mkatende haki;kwa maana wokovu wangu u karibu kuja na haki yangu kufunuliwa.Na wageni,walioambatana na Bwana ili wamhudumu,na kulipenda jina la Bwana,kuwa watumishi wake;kila aahikaye sabato asiivunje,na kulishika sana agano langu;Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu,na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala;makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu,kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.
Wimbo wa katikati Zab.67:1-2,4-5,7
1.Mungu na atufadhili na kutubaliki,
Nakuangazia uso wake.
Njia yake ijulikane duniani,
Wokovu wake katikati ya mataifa yote.
K:Watu na wakushuru,Ee Mungu,Watu wote na wakushukuru.
SOMO2:Rum.11:13-15,29-32
Nasema na ninyi,mlio watu wa Mataifa. Basi kwa kadri nilivyo mtume wa watu Mataifa,naitukuza huduma iliyo yangu?Huenda nikapata kuwatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi yao.Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu,je!kukubaliwa kwao kutakuwa na nini kama si uhai baada ya kufa.Kwasababu karama za Mungu hazina majuto,wala mwito wake.Kwa maana kama ninyi zamani mlivyo mwasi Mungu,lakini sasa mmepata rehema kwa kuasi kwao;Kadhalika na hao wameasi sasa,ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema.Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.
SHANGILIO Mdo.16:14
Aleluya,Aleluya
Fungua mioyo yetu,Ee Bwana,ili tuyatunze maneno ya Mwanao.
Aleluya.
INJILI:Mt.15:21-28
Yesu aliondoka huko,akaenda kando za Tiro na Sidoni.Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi;binti yangu amepagawa sana na pepo.Wala yeye hakumjibu neno.Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema,Mwache aende zake;kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.Akajibu,akasema,Sikutumwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Naye akaja akamsujudia, akisema, Bwana unisaidie.Akajibu akasema si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.Ndipo yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa;na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.

No comments: