MASOMO YA LEO ALHAMISI AGOSTI 3 2017 JUMA LA 17 LA MWAKA
SOMO1:Kut.40:16-21,34-38.
Musa alifanya hayo yote;kama yote Bwana alivyoagiza ndivyo alivyofanya. Hata mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili,siku ya kwanza ya mwezi,ile maskani,ilisimashwa.Musa akaisimisha maskani,akayaweka matako yake,akazisimamisha mbao zake akayatia mataruma yake,akazisimasha nguzo zake.Akaitanda hema juu ya maskani,akakitia kifuniko cha hema juu yake;kama Bwana alivyomwamuru Musa.Akautwaa ule ushuhuda,akautia ndani ya sanduku,akakiweka kiti cha rehema juu ya sanduku;kisha akalileta sanduku akalitia ndani ya maskani,naye akalitundika pazia la stara,akalisitiri sanduku la ushuhuda;kama Bwana alivyomwamuru Musa ndipo lile wingu likaifuniza hema ya kukutania,na huo utukufu wa Bwana akaujaza hema ya kukutania,na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani.Wala Musa hakuweza kuliingia hema la kukutania,kwa sababu lile wingu lilikaa juu yake,na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani.Hapo lile wingu lilipoinuliwa kutoka juu ya maskani,wana wa Israeli wakaenda mbele katika safari zao zote,bali kama lile wingu halikuinuliwa,wakati ule hawakusafiri hata siku ile lilipoinuliwa tena.Kwa maana lile wingu la Bwana lilikuwa juu ya maskani wakati wa mchana,na mlikuwa na moto ndani yake wakati wa usiku,mbele ya macho ya nyumba ya Israeli katika safiri zao zote.
K:Maskani zako zapendeza kama nini,ee Bwana wa majeshi-Zab.84:2-5,7,10.
INJILI:Mt.13:47-53
Yesu aliwaambia wanafunzi wake:Ufalme wa mbinguni umefanana na juya,lililotupwa baharini,likakusanya wa kila namna;hata lilipojaa,walivuta pwani;wakaketi,wakakusanya walio wema vyomboni,bali walio wabaya wakawatupa.Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia;malaika watatokea,watawatenga waovu mbali na wenye haki,na kuwatupa katika tanuru ya moto;ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.Yesu aliwauliza,Mmeyafahamu hayo yote? Wakawambia,Naam.Akamwambia,kwa sababu hiyo,kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.Ikawa Yesu alipoimaliza mifano hiyo,alitoka akaenda zake.

No comments: