MASOMO SIKUKUU YA MT.BARTOLOMEO MTUME ALHAMISI 24 AGOSTI 2017
SOMO1:Ufu.21:9-14
Malaika alinijia akanena nami,akisema,njoo huku nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi,mke wa Mwana-kondoo.Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa,mrefu,akanionyesha ule mji mtakatifu,Yerusalemu,akishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;wenye utukufuwa Mungu,na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi,safi kama bilauri;ulikuwa na ukuta mkubwa,mrefu,wenye milango kumi na miwili,na katika ile milango malaika kumi na wawili,na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli.Upande wa mashariki milango mitatu;na upande wa kaskazini milango mitatu;na upande wa kusini milango mitatu;na upande wa magharibi milango mitatu. Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili,na katika ile misingi majina kumi na mawili wa wale mitume kumi na wawili wa Mwana-kondoo.
K:Wacha Mungu wataunena utukufu wa ufalme wako,Ee Bwana. -Zab.145:10-13,17-18
INJILI:Yn.1:45-51
Filipo alimwona Nathanaeli,akamwambia,Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati,na manabii,Yesu,mwana wa Yusufu,mtu wa Nazareti.Nathanaeli akamwambia,Laweza neno jema kutoka Nazareti?Filipo akamwambia,Njoo uone.Basi Yesu,akamwona Nathanaeli anakuja kwake,akanena habari zake Tazama,Mwisraeli kwelikweli,hamna hila ndani yake . Nathanaeli akamwambia,umepataje kunitambua?Yesu akajibu,akamwambia,kabla Filipo hajakuita,ulipokuwa chini ya mtini nilikuona Nathanaeli akamjibu,Rabi,wewe u Mwana wa Mungu,ndiwe mfalme wa Israeli. Yesu akajibu,akamwambia,kwa sababu nlikuambia,Nilikuona chini ya mtini,waamini?Utaona mambo makubwa kuliko haya.Akawaambia,Amini,amini,nawaambia,Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.

No comments: