HABARI

Habari:
Mkuu wa jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema kwamba uelewa wa watu katika kutambua namna jeshi hilo linavyofanya kazi zake ni mdogo kutokana na wanapo wakamata watu kwa tuhuma za makosa mbalimbali,kama za kugushi nyaraka ama uchochezi wa jambo fulani huonekana kama wanawaonea hivyo ni vema wakaelewa kwamba wao kama jeshi wanafanya kazi kwa taratibu za kisheria na kisha kuchunguza makosa hayo na wakishabaini kwamba mtu hana kosa basi taratibu zingine zinafuata.

IGP Sirro amesema wakati watu wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali wanapo fikishwa ndani ya jeshi hilo, jeshi hupata taarifa za kiitelijensia za watu hao ambazo zinahitaji upelelezi zaidi hivyo inakuwa vigumu kumwachia mtu anayetuhumiwa kwa makosa fulani halafu likaibuka lingine wakati wakiwa wamemshikilia.

No comments:

Powered by Blogger.