MASOMO LEO JUMANNE 1 AGOSTI2017 JUMA LA 17 LA MWAKA
SOMO 1:Kut.33:7-11,34:5-9,28
Desturi ya Musa ,ilikuwa kuitwaa ile hema,na kuikita nje ya marago mbali na hayo marago;akaita,Hema ya kukutania.Hata kila mtu aliyekuwa akitaka neno kwa Bwana,akatoka akaenda hata hema ya kukutania,iliyokuwa nje ya marago.Hata Musa alipotoka kuiendea ile hema,watu wote waliondoka wakasimama,kila mtu mlangoni pa hema yake,akamtazama Musa,hata alipokwisha kuingia hemani.Ikawa Musa alipoingia humo hemani,ile nguzo ya wingu ikashuka,ikasimama mlangoni pa ile hema;naye Bwana akasema na Musa.Watu wote wakaiona nguzo ya wingu ikisimama penye mlango wa hema;watu wote wakaondoka wakasujudu,kila mtu mlangoni pa hema yake.Naye Bwana akasema na Musa uso kwa uso,kama mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata maragoni;bali mtumishi wake Yoshua,Mwana wa Nuni,naye ni Kijana hakutoka mle hemani. Bwana akashuka ndani ya lile wingu,akasimama pamoja naye huko,akalitangaza jina la Bwana.Bwana akapita mbele yake akatangaza bwana,bwana,Mungu mwingi wa huruma,mwenye fadhili,si mwepesi wa hasira,mwingi wa rehema na kweli;mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu,mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi;wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe;mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao,na wana wa wana wao pia,hata kizazi cha tatu na nne.Musa akafanya haraka,akainamisha kichwa chake hata nchi,akasujudu.Akasema,ikiwa sasa nimepata neema mbele zako,Bwana nakuomba,Bwana,uende kati yetu,maana ni watu wenye shingo ngumu;ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu,ukatutwae tuwe urithi wako.Naye alikuwa pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake;hakula chakula,wala hakunywa maji.Naye akaandika katika hizo mbao,hayo maneno ya maagano,hizo amri kumi.
K:Bwana amejaa huruma na neema.-Zab. 103:6-13
INJILI:Mt.13:36-43
Yesu aliwaaga makutano,akaingia nyumbani;wanafunzi wake wakamwendea,wakasema,Tufafanulie mfano wa magugu kondeni.Akajibu,akasema,Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu;lile konde ni ulimwengu;zile mbegu njema ni wana wa ufalme;na yale magugu wana wa yule mwovu;yule adui aliyepanda ni ibilisi;mavuno ni mwisho wa dunia.Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake,nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote,na hao watendao maasi,na kuwatupa katika tanuru ya moto;ndiko kutakuwako kilio cha kusaga meno.ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao.Mwenye masikio,na asikie.

No comments: