VIONGOZI WA KIDINI WATAKIWA KUSHIRIKIANA



Viongozi  wa  makanisa  hapa  nchini wametakiwa kuwa  na umoja ili kujenga umoja  wa  makanisa utakaomfanya Kristo  ahubiriwe kila  mahali kwa ukombozi  wa  watu  wote .

Hayo  yamesemwa   na  Askofu   John Mwakyusa  wa  Kanisa  la  FPTC, Jimbo la  Tanga hivi karibuni katika mahubiri yake.

Askofu Mwakyusa    amesema    kuwa  umoja  wa  makanisa  katika kuinjilisha ndiyo  msingi  kwa  neno  la  Mungu  na kuwa  siku   zote  kama   hakuna    umoja  hakuna   Kanisa. Amebainisha kuwa waamini  wakikaa  kwa  umoja  hata  nchi ni  rahisi  kukaa kwa  umoja kwa sababu misingi  yake ipo mioyoni mwa  watu wake.

No comments:

Powered by Blogger.