MASOMO YA LEO JUMA LA 14 LA MWAKA

Somo 1:Mwa.32:22-32
Yakobo aliondoka usiku ule akatwaa wakeze wawili,na vijakazi wake wawili,na wanawe kumi na mmoja akavuka kivuko cha Yokobi.Akawatwaa,akawavusha mto,akavusha na vyote walivyokuwa navyo.Yakobo akakaa peke yake;na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.Naye alipoona ya kuwa hamshindi,alimgusa panapo uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.Akasema,sikuachi usiponibariki.Akamuuliza,nina lako ni nani? Akasema,Yakobo.Akamwambia,jina lako hutaitwa tena Yakobo,ila Israeli,maana umeshindana na Mungu na watu,nawe umeshinda.Yakobo akamwuliza akasema,niambie tafadhali,jina lako?Akasema kwanini waniuliza jina langu?Akambariki huko.Yakobo akapita mahali pale,Penueli,maana alisema,Nimeonana na Mungu uso kwa uso,na nafsi yangu imeokoka.Jua likamzukia akivuka Penueli akachechemea kwa sababu ya paja la mguu wake.Kwahiyo wana wa Israeli hawali ule mshipa ulio katika uvungu wa paja hata leo;maana alimgusa Yakobo panapo uvunguni wa paja katika mshipa wa kiuno.

K:Nikutazame uso wako katika haki-zab.17:1-3,6-8,15

Injili:Mt.9:32-39
Walimletea Yesu mtu bubu mwenye pepo.Na pepo alipotolewa,yule bubu alinena,makutano wakastaajabu,wakasema,Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wowote.Lakini Mafarisayo wakasema,kwa nguvu za mkuu wa pepo atoa pepo.Naye yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji,akifundisha katika masinagogi yao,na kuihubiri habari njema ya ufalme,na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.Na alipowaona makutano,aliwahurumia,kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji,Ndipo alipo waambia wanafunzi wake,Mavuno ni mengi,lakini watendaji kazi ni wachache.Basi mwombeni Bwana wa mavuno,apeleke watenda kazi kqtika mavuno yake.

No comments:

Powered by Blogger.