MASOMO YA ALHAMISI 13 JULLY,2017

Somo1:Mwa.44:18-21,23-29,45:1-5

Yuda alimkaribisha Yusufu akasema,tafadhali,bwana wangu,mtumwa wako na aseme neno moja masikioni mwa bwana wangu,wala hasira yako isimwakie mtumwa wako,maana wewe u kama Farao.Wewe,bwana wangu,ulituuliza watumwa wako ukisema,Je,mnaye baba,au ndugu?Tukakuambia wewe,bwana wangu Tunaye baba,naye ni mzee,na mwana wa uzee wake ni mdogo,na nduguye amekufa;amebaki yeye peke yake wa katika tumbo la mamaye,na baba yake anampenda.Ukatuambia watumwa wako,mleteni kwangu,ili macho yangu yamwangalie.Asiposhuka ndugu yenu mdogo pamoja nami,hamtaniona uso wangu tena.Ikaww alipokwenda kwa mtumwa wako,baba yangu tukamwarifu maneno yako,bwana wangu.Kisha baba yetu akanena,rudini huko mkatununulie chakula kidogo.Tukasema,Hatuwezai kwenda;ndugu yetu mdogo akikuwepo pamoja nasi.Mtumwa wako,baba yangu akatuambia,mnajua ya kuwa mke wangu alinizalia wana wawili;mmoja alitoka kwangu,nikasema,bila shaka ameraruliwa,wala sikumwona tangu hapo.Na mkiniondolea huyu naye,na madhara yakimpata,mtashusha mvi zangu na msiba kaburini.Hapo Yusufu hawakuweza kujizuia mbele yao wote waliosimama karibu naye.Akapiga kelele na kisema,mwondokeni kila mtu mbele yangu.Wala hakusimama mtu pamoja naye.Yusufu alipojitambulishi kwa ndugu.Akapaza sauti yaka akalia,nao Wamisri wakasikia.Watu wa Nyumba ya Farao nao wakasikia.Yusufu akawambia ndugu zake,mimi ndimi Yusufu;baba yangu angali hai bado?Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu,maana waliingiwa na hofu mbele yake.Yusufu akawambia ndugu zake,karibuni kwangu;basi wakakaribia.Akasema,mimi ni Yusufu ,ndugu yenu,ambaye mliniuliza kwenda Misri.Basi sasa,msihuzunike,wala msihudhike nafsi zenu,kwa kuniuza huku Maana mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu.

K:Zikumbukeni ajabu Bwana alizozifanya.

Injili:Mt.10:7-15
Yesu aliwaambia mitume wake;katika kuenenda kwenu,hubirini, mkisema,Ufalme wa mbinguni umekaribia.Pozeni wagonjwa,fufueni wafu,takaseni wenye ukoma,toeni pepo,mmepata bure,toeni bure.Msichukue dhahabu,wala fedha,wala mapesa mishipini mwenu;wala mkoba wa safari,wala kanzu mbili,wala viatu,wala fimbo;maana mtenda kazi astahili posho lake.Na mji wowote au kijiji chovhote mtakachoingia,tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu;mkae kwake hata mtakapotoka.Nanyi mkiingia katika nyumba ya isalimuni.Na nyumba ile ikistahili,amani yenu na iifikilie;la,kwamba haistahili,amani yenu na iwarudie ninyi.Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu,mtokapo katika nyumba ile,au mji ule,kung'uteni mavumbi ya miguuni mwema.Amin,nawambia,Itakuwa rahisi nchi ya Sodoma na Gomora kustahili adhabu siku ya hukumu,kuliko mji ule.

No comments:

Powered by Blogger.