MASOMO YA LEO JUMATATU TAREHE 24 JULAI 2017 JUMA LA 16 LA MWAKA
SOMO1:Kut.14:5-18
Mfalme wa Misri aliambiwa ya kuwa wale watu wamekwisha kimbia;na moyo wa Farao na mioyo ya watumishi wake,iligeuzwa iwe kinyume cha hao watu,nao wakasema,Ni nini jambo hili tulilotenda,kwa kuwaacha Waisraeli waende zao wasitutumikie tena?Akaandali gari lake,akawachukua wwtu wake pamoja naye,tena akatwaa magari mia sita yaliyochaguliwa,na magari yote ya Misri,na maakida juu ya magari hayo yote.Na Bwana akaufanya moyo wake Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu,naye akawafuata wana wa Israeli;kwa sababu wana wa Israeli walitoka kwa ujeuri.Wamisri wakafuata nyuma yao,farasi zote na magari yote ya Farao,na askari zake wenye kupanda farasi,na jeshi lake,nao wakawapata hali wamepanga pale karibu na bahari, karibu na Pi-hahirothi,kukabili Baal-sefoni.Hata Farao alipokaribia,wana wa Israeli wakainua macho yao,na tazama,Wamisri wanakuja nyuma yao;wakaogopa sana;wana wa Israeli wakamlilia Bwana.Wakamwambia Musa,Je?,kwa sababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko ili tufe jangwani?Mbona umetutendea haya,kututoa katika nchi ya Misri?Neno hili silo tulilokuambia huko Misri,tukisema,tuache tuwatumikie Wamisri maana ni afadhali kuwatumikia wamisri kuliko kufa jangwani.Musa akawaambia watu,msiogope,simameni tu,mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo;kwa maana hao wamisri mliowqona leo hamtawaona tena milele.Bwana atawapigania ninyi,nanyi mtanyamaza kimya.Bwana akamwambia Musa,mbona unanililia mimi?Waamnie wana wa Israeli waendelee mbele.Nawe inua fimbo yako ukanyooshe mkono wako juu ya bahari,na kuigawanya;nao wana wa Israeli watapita kati ya bahari katika nchi kavu.Nami,tazama,nitaifanya mioyo ya wamisri kuwa migumu,nao wataingia na kuwafuatia,nami nitajipatia utukufu kwa Faro,na kwa jeshi lake lote,kwa magari yake na kwa wapanda farasi wake. Na wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana,nitakapokwisha kujipatia utukufu kwa Farao,na magari yake,na farasi zake.
K:Nitamwimbia Bwana,kwa maana ametukuka sana -Kut.15:1-6.
INJILI:Mt.12:38-42
Baadhi ya waandishi wa Mafarisayo walimjibu Yesu wakasema,Mwalimu,twataka kuona ishara kwako.Akajibu,akamwambia,kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara,wala hakitapewa ishara,ila ishara ya nabii Yona.Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi,hivyo ndivyo mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki,nao watawahukumu kuwa wamekosa;kwa sababu wao walitubu mahubiri ya Yona;na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona.Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki,naye atawahukumu kuwa wamekosa;kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani,na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.

No comments: