MASOMO YA LEO JUMANNE TAREHE 25 JULAI 2017 SIKUKUU YA MT.YAKOBO,MTUME

S0MO1:2Kor.4:7-15

Tuna hazina hii katika vyombo vya udongo,ili adhama Kuu ya uwezo iwe ya Mungu,wala si kutoka kwetu.Pande zote twadhihirika,bali hatusongwi;twaona shaka,bali hatukati tamaa;twaudhiwa,bali hatuachwi;twatupwa chini,bali hatuangamizwi;siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake yesu,ili uzima wa Yesu udhihirishwe katika miili yetu.Kwa maana sisi tulio hai,siku zote twatolewa ili tufe kwaajili ya Yesu,ili uzima wa Yesu nao udhihitishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti.Basi mauti hapo hufanya kazi ndani yetu,bali uzima ndani yenu.Lakini kwakuwa tuna roho ileile ya imani;kama ilivyoandikwa,Naliamini,na kwasababu hiyo nalinena;tukijua ya kwamba yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua na sisi nasi pamoja na Yesu,na kutuhudhurisha pamoja nanyi.Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu,ili neema hiyo ikiongezwa sana kwa hao walio wengi shukrani izidishwe,na Mungu atukuzwe.

K:Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha.-Zab.126

INJILI:Mt.20:20-28

Mama yao wana wa Zebadayo alimwendea Yesu pamoja na wanawe,akamsujudia,na kumwomba neno.Akamwambia,wataka nini?akamwambia,Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wa kuume,na mmoja mkono wako wa kushoto,katika ufalme wako.Yesu akajibu akasema,Hamjui mnaloomba.Je!mwaweza kunywea kikombe changu;lakini kuketuli mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto,sina amri kuwapa,bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.Na wale kumi wasiposikia,waliwakasirikia wale ndugu wawili.Lakini yesu akawaita akasema,Mwajua ya kuwa wakuu wa mataifa huwatawala kwa nguvu,na wakubwa wao huwatumikisha.Lakini haitakuwa hivyo kwenu;bali mtu yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu,na awe mtumishi wenu;na mtu anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa,bali kutumika,na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.

No comments:

Powered by Blogger.