MASOMO YA LEO JUMATANO TAREHE 26 JULAI 2017 JUMA LA 16 LA MWAKA
Somo1:Kut.16:1-5,9-15
Walisafiri kutoka Elimu,na mkutano wote wa wana wa Israeli wakafikilia bara ya Sini,iliyoko kati ya Elimu na Sinai,siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili baada ya kutoka kwao nchi ya Misri.Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawanung'ukia Musa na Haruni,huko barani;wana wa Israeli wakawambia,laiti tungalikufa kwa mkono wa Bwana katika nchi ya Misri,hapo tulipoketi karibu na sufuria za nyama,tulipokula vyakula hata kushiba;kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hili,ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili lote.Ndipo bwana akamwambia Musa,Tazama,Mimi nitawanyeshea ninyi mvua ya mkate kutoka mbinguni;na hao watu watatoka nje na kuokota kila siku sehemu ya siku ya sita,ya kwamba watayaandaa hayo watakayoleta ndani, nayo yatakuwa ni mara ya mbili kuliko wayaokotayo kila siku.Musa akamwambia Haruni,Haya,sema na mkutano wote na wana wa Israeli.Njooni karibu mbele ya Bwana;kwakuwa yeye ameyasikia manung'uniko yenu.Ilikua Haruni aliponena na huo mkutano wote wa wana wa Israeli wakaangalia upande wa bara,na tazama,utukufu wa Bwana ukaonekana katika hilo wingu.Bwana akasema na Musa,akinena, Nimeyasikia manung'uniko ya wana wa Israeli;haya!Sema nao,ukinena,Wakati wwa jioni mtakula nyama,na wakati wa subuhi mtashiba mkate;nanyi mtajua kuwa mimi ndimi Bwana,Mungu wenu.Ikawa wakati wa jioni;kware wakakaribia,wakanifunikiza kituo;na wakati wa asubuhi umande ulikua juu ya nchi pande zote za kituo.Na ulipoinuka ule umande ulikua juu ya nchi,kumbe!Juu ya uso wa bara kitu kidogo kilichoviringana,kidogo kama sakitu juu ya nchi.Wana wa Israeli walipokiona,wakaambiana,nini hiki?Maana hawakujua ni kitu gani.Musa akawaambia,Ndio mkate ambao bwana amewapa ninyi,mle.
K:Bwana aliwapa nafaka ya mbingu.-78:18-19,23-28
INJILI:Mt.13:1-9
Yesu alitoka nyumbani,akaketi kando ya bahari.Wakamkusanyikia makutano mengi,hata akapanda chomboni,akaketi na ule mkutano wote wakasimama pwani.Akawaambia mambo mengi kwa mifano,akisema,Tazama,mpanzi alitoka kwenda kupanda.Hata alipokuwa akipanda,mbegu nyingine zilianguka karibu na njia,ndege wakaja wakazila;nyingine zikaanguka penye miamba,pasipokuwa na udongo mwingi;mara zikaota,kwa udongo kukosa kina;na jua lilipozuka ziliungua;na kwakuwa hazina mizizi zikanyauka.Nyingine zikaanguka penye miiba;ile miiba ikamea,ikazisonga;nyingine zikaanguka penye udongo mzuri,zikazaa,moja mia,moja sitini,moja thelathini.Mwenye masikio na asikie.

No comments: