MASOMO YA LEO IJUMAA TAREHE 28 JULAI 2017
SOMO 1:Kut.20:1-17
Mungu alinena maneno haya yote akasema,Mimi ni Bwana,Mungu wako,niliyekutoka katika nchi ya Misri,katika ya utumwa.Usiwe na miungu ila mimi. Usijifanye sanamu ya kuchonga,wala mfano kitu chochote kilicho juu mbinguni,wala kilicho chini ya dunia.Usivisujudie wala kuvitumikia;kwa kuwa mimi,Bwana,Mungu wako,ni Mungu mwenye wivu;nawapatiliza wana maovu ya baba zao,hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao,na kuzishika amri zangu.Usilitaje bure jina la Bwana,Mungu wako,maana bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.Ikumbuke siku ya sabato uitakase.Siku sita fanya kazi,utende mambo yako yote;lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana,Mungu wako,siku hiyo usifanye kazi yeyote,wewe,wala mwana wako,wala binti yako,wala mtumwa wako,wala mjakazi wako,wala mnyama wako wa kufuga,wala mgeni aliye ndani ya malango yako.Maana,kwa siku sita bwana alifanya mbingu, na nchi,na bahari,na vyote vilivyomo,akastarehe siku ya saba;kwahiyo Bwana akaibariki siku ya sabato akaitakasa.Waheshimu bababa yako na mama yako;siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana,Mungu wako.Usiue.Usizini.Usiibe.Usimshuhudie jirani yako uongo.Usiitamani nyumba ya ya jirani yako,usitamani mke wa jirani yako;wala mtumwa wake,wala mjakazi wake,wala ng'ombe wake,wala punda wake,wala chochote alichonacho jirani yako.
K:Bwana,unayo maneno ya uzima wa milele.-Zab 19:8-11(K)Yn 6:68
INJILI:Mt.13:18-23
Yesu aliwambia Wanafunzi wake:Ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi.Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo,huja yule mwovu,akalinyakua lililopandwa moyoni mwake.Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.Naye aliyepandwa penye miamba,huyo ndiye alisikiaye lile neno,au udhia kwa ajili ya lile neno,mara huchukizwa.Naye aliyepandwa penye miiba,huyo ndiye alisikiaye lile neno;na shughuli za dunia,na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno;likawa halizai.Naye aliyepandwa penye udongo mzuri,huyo ndiye alisikiaye lile neno,na kuelewa nalo;yeye ndiye azaaye matunda,huyu mia,na huyu sitini,na huyu thelathini.

No comments: