MASOMO YA DOMINIKA YA 17 YA MWAKA A TAREHE 30 JULAI 2017.

SOMO1:1Fal.3:5,7-12

Huko Gibeoni Bwana alimtokea Sulemani katika ndoto ya usiku;Mungu akamwambia,Omba utakalo nikupe.Suleimani akasema,Ee Bwana,Mungu wangu,umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu;nami ni mtoto mdogo tu;sijui na jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia.Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua,watu wengi wasioweza kuhesabiwa,wala kufahamiwa idadi yao,kwa kuwa ni wengi.Kwahiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako,na kupambanua mema na mabaya;maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?Neno hili likawa jema machoni pa Bwana,ya kuwa Sulemani ameomba neno hili.Mungu akamwambia,kwa kuwa umeomba neno hili wala hukujitakia maisha ya siku nyingi;wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako;wala hukutaka roho za adui zako;bali umejitakia akili za kujua kuhukumu;basi,tazama,nimefanya kama ulivyosema.Tazama,nimekupa moyo wa hekima na wa akili;hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe,wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.

Wimbo wa katikati Zab.118:57,72,76-77,127-130.



SOMO 2:Rum.8:28-30

Twajua yakuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale waampendao katika k uwapatia mema,yaani,wale walioitwa kwa kusudi lake.Maana wale aliowajua tangu asili,aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wale,ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.Na wale waliochaguliwa tangu asili,hao akawaita;na wale aliowaita,hao akawahesabia haki;na wale aliowahesabia haki,hao akawatukuza.


INJILI:Mt.13:44-52

Yesu aliwambia wafuasi wake:Ufalme wa mbinguni umefanana na  hazina iliyositirika katika shamba;ambayo mtu alipoiona,aliificha,na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote,akalinunua shamba lile. Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanyabiashara,mwenye kutafuta lulu nzuri;naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa,alikwenda akauza alivyo navyo vyote,akainunua.
Tena ufalmebwa mbinguni umefanana na juya,lililotupwa baharini,likakusanywa wa kila namna;hata lilipojaa,walivuta pwani;wakaketi,wakakusanya walio wema vyomboni,bali walio wabaya wakawatupa.Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia;malaika watatokea,watawatenga waovu mbali na wenye haki,na kuwatupa katika tanuru ya moto;ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.Yesu aliwauliza,Mmeyafahamu hayo yote?Wakawambia,Naam.Akamwambia,kwa sababu hiyo,kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina ya vitu vipya na vya kale.

No comments:

Powered by Blogger.