MASOMO YA LEO IJUMAA JUMA LA 14 LA MWAKA

SOMO1:Mwa.46:1-7,28-30

Israeli alisafiri pamoja na yote aliyokuwa nayo,Beer-sheba,akamchinja sadaka Mungu wa Isaka babaye.Mungu akanena na Israel katika ndoto ya usiku,akasema,Yakobo,Yakobo.Akasema Mimi hapa.Akasema Mimi ni Mungu,Mungu wa baba yako,usiogope kushuka mpaka Misri;maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko.Mimi nitashukuka pamoja nawe mpakaMisri;nami nitakupandisha tena bila shaka;na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako.Yakobo akaondoka,kutoka Beer-sheba;wana wa Israeli wakamchukua baba yao na watoto wao wadogo,na wake zao katika magari aliyoyapeleka Farao ili kumchukua.Wakatwaa na wanyama wao,na mali zao walizokua wamezipata katika nchi ya kaanani wakaja Misri,Yakobo na uzao wake wote pamoja naye.Wanawe,na wana wa wanawe,pamoja naye,binti zake na binti za wanawe,na uzao wake wote,aliwaleta pamoja naye mpaka Misri.Yakobo akampeleka Yuda mbele yake Yusufu,ili amwongoze njia mpaka Gosheni.Wakaja mpaka nchi ya Gosheni Yusufu akatandika gari lake,akapanda kwenda kumlaki Israeli,babaye,huko Gosheni;akajionyesha kwake,akamwangukia shingoni,akalia shingoni mwake,kitambo kizima.Israeli akamwambia Yusufu,Na nife sasa,kwa kuwa nikuona uso wako,ya kuwa ungali hai.

K:Wokovu wa wenye haki una bwana.-Zab.37:3-4,18-19,27-28,39-40

Injili:Mt.10:16-23

Yesu aliwambia mitume wake:Angalieni,mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu;basi iweni na busara kama nyoka,na kuwa watu wapole kama hua Jihadharini na wanadamu;kwa maana watapeleka mabarazani,na katika masinagogi yao watawapiga;nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwaajili yangu,kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.Lakini hapo watakapowapeleka,msifikiri fikiri mtakavyosema;Maana mtapewa saa ile mtakayosema.Kwakuwa si ninyi msemao,bali ni Roho wa baba yenu asemaye ndani yenu.Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe,na baba atamsaliti mwana,na wana watainukia wazazi wao,na kuwafisha.Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu kwa ajili ya jina langu;lakini mwenye kuvumilia hata mwisho,ndiye atakayeokoka.Lakini watakapowafukuza katika mji huu,kimbilieni mwingine;kwa maana ni kweli nawaambia,Hamtaimaliza miji ya Israeli,hata ajapo Mwana wa Adamu.

No comments:

Powered by Blogger.