MASOMO YA JUMAPILI DOMINIKA YA 15 YA MWAKA

Somo1:Isa.55:10-11

Kama vile mvua ishukayo,na theluji,kutoka mbinguni,wala hairudi huko;bali huinyesha ardhi,na kuizalisha na kuichipuza,ikampa mtu apandaye mbegu,na mtu alaye chakula;ndivyo litakavyo kuwa neno langu,litokalo katika kinywa changu;halitanirudia bure,bali litatimiza mapenzi yangu,nalo litafanikiwa katika yale niliyotuma.

Wimbo wa katikati Zab.65:9-13

1.Umeijilia nchi na kustawisha,
   Mto wa Mungu umejaa maji;
  Wawazuruku watu nafaka
  Maana ndiwe uitegemezaye ardhi.

K:Mbegu nyingine zikaanguka penye udongo mzuri zikamea,zikazaa.

2.Matuta yake yawajaza maji;
Wapasawazisha palipoinuka,
Wailainisha nchi kwa manyunyu;
Wainariki mimea yake(k)
3.Umuuvika mwaka taji ya wema wako;
Mapito yako yadondoza unono,
Huyadondokeza malisho ya nyikani.
Na vilima vyaifunga furaha.(k)
4.Na malisho yamevikwa kondoo,
Na mabonde yamepambwa nafaka,
Yanashangilia,naam,yanaimba.(k)

SOMO 2:Rum.8:18-23

Ndugu,nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu
ule utakaofunuliwa kwetu.Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu.Kwa maana viumbe vyote pia viliitishwa chini ya ubatili;si kwa hiari yake,ila kwa sababu yake yeye aliyeviitisha katika tumaini;kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu;hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja,navyo vina utungu pamoja hata sasa.Wala si hivyo tu;ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho,sisi poa tunaugua katika nafsi zetu,tukikitazamia kufanywa wana,yaani ukombozi wa mwili wetu.

              SHANGILIO Efe.1:17,18

Aleluya,Aleluya.
Baba wa Bwana wetu Yesu kristo,uyatiae nuri macho ya mioyo yetu,
Ili tujue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo.
Aleluya.


INJILI:Mt.13:1-23

Siku ile yesu alatoka,nyumbani akaketi ya bahari.Wakamkusanyia makutano chomboni,akaketi;ule mkutano wote wakasimama pwani.Akawambia mambo mengi kwa mfano,akisema Tazama mpanzi alitoka kwenda kupanda.Hata alipokuwa akipanda,mbegu nyingine zilianguka karibu na njia,ndege wakaja wakazila;nyinyine zikaanguka katika miamba,pasipokuwa na udongo mwingi;mara zikaota,kwa udongo kukosa kina,na jua lilipozuka ziliungua;na kwakuwa hazina mizizi zilinyauka.Nyingine zilianguka Katika miiba;ile miiba ikamea,ikazisonga,nyingine zikaanguka penye udongo mzuri,zikazaa,moja mia,moja sitini,moja thelathini.Mwenye masikio na asikie.Wakaja wanafunzi wakamwambia,kwanini wasema nao kwa mifano?Akajibu,akamwambia,Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za mbinguni,bali wao hawakujaliwa.Kwa maana yeyote mwenye kitu atapewa,naye atazidishiwa tele,lakini yeyote asiye na kitu,hata kile alichonacho atanyang'anywa.Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano;kwa kuwa wakitazama hawaoni,na wakisikia hawasikii,wala kuelewa.Na neno la nabii Isaya linatimia kwao,likisema,kusikia mtasikia,wala hamtaelewa;kutazama mtatazama,wala hamtaona,Maana mioyo ya watu hawa imekua mizito,na kwa masikio yao hawasikii vyema,Na macho yao wameyafumba;wasije wakaona kwa macho yao,wakasikia kwa masikio yao,wakaelewa kwa mioyo yao,wakaongoka,nikawaponya.Lakini heri macho yenu,kwa kuwa yanaona;na masikio yenu,kwakuwa yanasikia.Kwa maana,amin,nawaambia,Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi,wasiyaone;na kuyasikia mnayoyaaikia ninyi msiyasikie.
Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi.Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo,huja yule mwovu,akalinyakua lililopandwa moyoni mwake.Huyo ndiye alioandwa karibu na njia.Naye aliyepandwa penye miamba,huyo ndiye alisikiaye lile neno,akalipokea mara kwa furaha;lakini hana mizizi ndani yake ,bali hudumu kwa muda,ikitokea dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno mara huchukizwa.Naye aliyepandwa penye miiba,huyo ndiye alisikiaye lile neno;na shughuli za dunia,na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno;likawa halizai.Naye aliyepandwa penye udongo mzuri,huyo ndiye alisikiaye lile neno,na kuelewa nalo;yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia,na huyu sitini,na huyu thelathini.













































No comments:

Powered by Blogger.