DOMINIKA YA 14 YA MWAKA (Mwaka A)

   Sala ya Asubuhi.
Ee baba yetu Mungu mkuu,
Umenilinda usiku huu,
Nakushukuru kwa moyo,
Ee Baba mwana na roho.

Nilinde tena siku hii,
Niache dhambi,nikutii,
Naomba sana baba wee
Baraka yako nipokee.

Bikira safi, Ee maria,
Nisipotee nisimamie,
Mlinzi mkuu malaika wee
Kwa Mungu wetu niombee,nitake,nitende mema tu
Na mwisho nije kwako juu.Amina.

  Nia njema.
Kumheshimu Mungu wangu
Namtolea roho yangu,
Nifanye kazi nipumzike,
Amri zako tu nishike.

Wazo,neno,tendo yote
Namtolea mungu pote.
Roho,mwili,chote changu,
Pendo na uzima wangu.

Mungu wangu nitampenda,
Wala dhambi sitatenda
Jina lako nasifia,
Utakalo hutimia.

Kwa utii navumilia
Teso na matata pia
Nipe,Bwana,neema zako
Niongeze sifa yako.Amina.

Amri za Mungu
1.Ndimi bwana mungu wako,
   Usiabudu miungu wengine.
2.Usilitaje bure jina la mungu wako.
3.Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4.Waheshimu baba na mama,upate.          miaka mingi na heri duniani.
5.Usiue
6.Usizini
7.Usiibe
8.Usiseme uongo
9.Usitamani mwanamke asiye mke.         wa.ko.
10.Usitamani mali ya mtu mwingine.


          Amri za kanisa
1.Hudhuria misa takatifu jumapili na sikukuu zilizoamriwa.
2.Funga siku ya jumatano ya Majivu,
Usile nyama siku ya ijumaa kuu.
3.Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka.
4.Pokea Ekaristi takatifu hasa wakati wa paska.
5.Saidia kanisa katoliki kwa zaka.
6.Shika sheria katoliki za ndoa.


DOMINIKA YA 14 YA MWAKA(MwakaA)

Somo 1:zek.9:9-10.
Furahi sana,Ee binti sayuni;Piga kelele,Ee binti Yerusalemu;Tazama,mfalme wako anakuja kwako,Ni mnyenyekevu,amepanda punda,Naam,mwana punda,mtoto wa punda.Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu,na farasi awe mbali na Yerusalemu,na upinde wa vita utaondolewa mbali;naye atawahubiri mataifa yote habari za amani;na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari,natoka Mto hata miisho ya dunia.

Wimbo wa katikati zab.145:1-2,8-11,14,17.

1.Ee Mungu wangu,Mfalme,nitakutukuza,
Nitalihimidi jina lako milele na mikee.
Kila siku nitakuhimidi,Italisifu jina lako milele na milele.

K:Nitalihimidi jina lako milele na milele.

2.Bwana ana fadhili,ni mwingi wa huruma,Si mwepesi wa hasira,ni mwingi wa rehema.
Bwana ni mwema kwa Watu wote
,Na rehemu zake zi juu ya kazi zake zote.(K)

3.Ee Bwana,kazi zako zote zitashuru,
Na wacha Mungu wako wakakuhimidi.
Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza wako.(K)

4.Bwana ni mwenyewe haki katika njia zake zote,
Na mwenyewe fadhili juu ya kazi zake zote.Bwana huwategemeza wote waanguka,Huwainua wote walioinama chini.(K)

Somo 2:Rum.9,11-13

Roho wa Mungu anakaa ndani yenu,ninyi hamwufuati mwili;bali mwaifuata roho.Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa kristo,huyo si wako.lakini,ikiwa Roho wake yenye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu,yeye aliyemfufua kristo Yesu katika wafu ataihusisha na miili yenu iliyo katika hali kufa,kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.Basi,kama ni hivyo,ndugu,tu wadeni,si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili;kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili,mwatakakufa;bali kama mkiyasha matendo ya mwili kwa Roho,mtaishi.

Shangilio 1sam.3.9;Yn.6:68
        Aleluya,aleluya,
Nena Bwana,kwa kuwa mtumishi wako anasikia;wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
       Aleluya.

Injili:Mt:25-30.
Wakati ule Yesu alijibu,akasema,Nashukuru,Baba,Bwana wa mbingu na nchi,kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili,ukawafunulia watoto wachanga.Naam,Baba,kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.Akasema,Nimekabidhiwa vyote na baba yangu;wala hakuna amjuaye Mwana,ila Baba;wala hakuna amjua baba,ila Mwana,na yeyote ambaye mwana apenda kumfunulia.Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo,nami nitawapumzisha.Jitieni nira yangu,mjifunze kwangu;kwa maana nira yangu Ni laini,na mzigo wangu ni mwepesi.Neno la bwana.

1 comment:

Powered by Blogger.