TUUTAFAKARI PAMOJA UJUMBE WA MASOMO YA LEO.

Somo1:Mwa.28:10-22
Yakobo alitoka Beer-sheba,kwenda Harani.Akafika mahali fulani akakaa usiku kucha,maana jua lilikua lomekuchwa;akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake,akalala usingizi pale pale.Akaota ndoto,na tazama,ngazi imesimamisha juu ya nchi,na ncha yake yafika mbinguni.Tena,tazama,malaika wa Mungu wwnapanda,na kushuka juu yake.Na Tazama bwana amesimama juu yake,akasema,Mimi ni Bwana,Mungu wa Ibrahimu baba yako,na Mungu wa Isaka;nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wwko.Na uzao wako utakuwa kqma mavumbi ya nchi,nawe utaenea upande wa magharibi,na mashariki,na kaskazini,na kuaini;na katika wewe,na katika uzao wako,jamaa zote za dunia watabarikiwa.Na tazama mimi nipo pamoja nawe,nitakulinda kila uendako,nami nitakuleta tena mpaka nchi hii,kwa maana sitakuacha,hata nitakapo kufanyia hayo niliyokuambia.Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema,kweli,Bwana yupo mahali hapa,wala mimi sikujua.Naye akaogopa akasema,mahali hapa pana tisha kama nini!Bila shaka,hapa ni nyumba ya Mungu,napo ndipo lango la mbinguni.Yakobo akaondoka asubuhi na mapema akalitwaa lile jiwe aliloweka chini ya kicwa chake,akalisimamisha kama nguzo,na kumimina mafuta juu yake.Akaita jina la mahali pale Betheli;lakini jinala mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.Yakobo akaweka nadhiri akisema,Mungu akiwa pamoja nami,akinilinda katika njia niiendeayo,na kunipa chakula nile,na nguo nivae;nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu,ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu.Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo litakuea nyumba ya Mungu;na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.

K:Mungu wangu nitakaye mtumainia.-Zab.91:1-4,14-15.

Injili:Mt.9:18-26
Yesu aliokuwa akiwaambia hayo,tazama,akaja jumbe mmoja,akamsujudia,akisema,Binti yangu sasa hivi amekufa;lakini njoo,uweke mkono wako juu yake,naye ataishi.Akaondoka Yesu,akamfuata,pamoja na wanafunzi wake.Na tazama,mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili,alikuja kwa nyuma,akagusa upindo wa vazi lake.Kwa maana alisema moyoni mwake,Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona.Yesu akageuka,akamwona,akamwambia,Jipe moyo mkuu,binti yangu,imani yako itakuponya.Yule mwanamke akapona tangu saa ile.Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe,aliona wapiga filimbi,na makutano wakifanya maombolezo,akawaambia,ondokeni;kwa maana kijana hakufa amelala tu.Wakamcheka sana.Lakini makutano walipoondoshwa,aliingia,akamshika mkono;yule kijana akasimama.Zikaenea habari hizi nchi ile yote.

Tuombe,
Ee Yesu mwema mno,nakuangukia nikiomba nataka sana,upende kutia moyoni mwangu imani na matumaini na mapendo yako.Unifanye nitubu kweli dhambi zangu,nitake sana kugeuza mwenendo wangu.Ndio hayo ninayokuomba sasa,niwazapo,ninapoangalia kwa akili yangu,madonda yako matano,kwa kuikitikia sana moyoni,na kukuonea huruma,nikikumbuka maneno aliyonena Nabii Daudi juu yako,akisema:"Wakanitoboa mikono na miguu,wakahesabu mifupa yangu yote".

Baba yetu×3
Salamu Maria×3
Atukuzwe Baba×3.

No comments:

Powered by Blogger.